fbpx
Gari, Teknolojia

Mabetri ya gari la BMW i3 kutumika kwa ajili ya umeme wa majumbani

betri-gari-bmw-kuzalisha-umeme-majumbani
Sambaza

Mabetri yasiyofaa tena kutumika kwa ajili ya kuendeshea magari ya umeme yafanywaje? BMW wamekuja na kazi nzuri kwa ajili ya mabetri hayo.

BMW ambao ni maarufu katika utengezaji wa magari, pikipiki na vifaa vya magari waamua kutumia betri ambazo haziwezi tena kutumika kwenye gari na kutumika katika umeme wa majumbani.

Mwaka 2009 BMW iliamua kutengeneza gari aina ya BMW i3 zenye kutumia umeme(electric cars) ambazo zimekuwa zikiuzika duniani kote kwa sababu hazili umeme sana, muonekano wake ni mzuri na sio ghali sana.

INAYOHUSIANA  Antonov An - 225 Ifahamu ndege Kubwa Zaidi Duniani! #Teknolojia
Fari aina ya BMW i3
Gari aina ya BMW i3

Hivi karibuni BMW wametangaza kuwa betri za gari i3 ambazo zimekwisha nguvu zimebadilishwa matumizi na kuweza kutumika kuwasha umeme wa majumbani. Betri za ina mbili; moja inazalisha 22kWh na nyingine 33kWh.

Kwa Marekani inasemakana kwa siku nyumba moja inatumia kiwango cha umeme cha kati ya kWh 15-30 na hivyo kupitia betri hizi mtu ataweza kupata takribani masaa 24 ya umeme wa ziada pale umeme ukikatika.

Betri inayotumika kwenye BMW i3 kutumika kama chanzo cha umeme wa majumbani
Betri inayotumika kwenye BMW i3 kutumika kama chanzo cha umeme wa majumbani

Betri hizo zina uwezo wa kubadilisha volti(voltage converter) ili kuweza kudhibiti umeme huo usiweze kuleta madhara majumbani. Pia, betri hizo zinaweza kutumika kuchaji betri nyingine ambayo inatumika kwenye gari linalotumia umeme.

Betri hizo zitaweza kuunganisha moja kwa moja na chanzo kingine cha umeme na hivyo kuweza kukupatia umeme ata pale ambapo umeme unaotegemewa umekatika. Inasemakana mahitaji ya nyumbani hayaitaji nguvu nyingi ya umeme kama ile inayoitajika kwenye gari la i3 na hivyo mabetri hayo yataweza kufanya kazi vizuri tuu na kwa muda mrefu.

INAYOHUSIANA  Obama atajua juu ya John Snow kabla yetu.

Nao kampuni ya Tesla mwaka 2015 ilitangaza kutumia betri zake ambazo zilikuwa zikitumika kwenye magari “Model S cars”. Hii ni mara ya kwanza kwa BMW kufanya aina hii ya biashara na imefahamika kuwa betri hizo zitaanza kuuzwa mwakani.

Soma kuhusu teknolojia na Magari -> Teknokona/Magari

Una lolote la kusema kuhusu makala hii? Comment hapo chini na mimi nitakujibu. Usiache kutembelea Teknokona kila siku kusoma habari mbalimbali kwa Kiswahili.

Chanzo: Extreme tech, Car AND Driver

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , , ,

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|