Virtual Assistant au mara nyingine intelligent personal assistant huwa ni programu au app ambazo zinatengenezwa na kupewa nguvu ya kufanya kazi mbalimbali endapo zikiamuriwa na watumiaji wa programu hizo kwa kutumia sauti.
Facebook wako katika utengenezaji wa programu hii. Ijapokua kampuni iko katika hatua za mwanzo mwanzo katika teknolojia hii, bado imeweka wazi bayana kuwa watu wasitegemee kuwa itaanza kushindana na Virtual Assistant zingine kama Alexa kutoka Amazon au ya Google inayofahamika kama Google Assistant. Wengi wanaamini Facebook M itakuwa ndani ya app na bidhaa zake zinazopatikana chini ya kampuni ya Facebook.
Nafikiri ni jambo zuri, kampuni inabidi kwanza ijikite katika kuhakikisha kuwa teknolojia hiyo inafika katika messenger. Ukiachana na teknolojia hii bado kuna vitu vingine ambavyo Facebook inavifanyia kazi kuhakikisha kuwa kuna matumizi macheche ya mikoni wakati watumiaji wakitumia mtandao na vifaa vyake (hands free).
Kumbuka hapo mwanzo kampuni ilitengeneza AI Assistant (msaidizi) kwa ajili ya messenger ambae alikua anaitwa M, na baadae wakafunga kitengo hicho, ila sasa wanakifua kivingine.
Facebook imesema kuwa inahangaika katika kutengeneza teknolojia za AI Assistant na Sauti ili kuhakikisha zitatumika katika bidhaa zake za AR/VR hii itajumuisha bidhaa kama Portal, Oculus na zingine zijazo.
Kwa sasa teknolojia hizi zina watumiaji wengi na matumizi yake ni makubwa sana kwani dunia inazidi kubadilika na watu wanazidi kuwa wavivu katika kutumia mikono yao.
Kwa kampuni ni jambo zuri na pia itawafanya watumiaji wa teknolojia hiyo kuvutiwa (kutumia kwa urahisi) zaidi na bidhaa za Facebook ambazo zinatumia teknolojia za AI.
Niambie wewe unaona ni jambo sahihi kabisa kwa sasa kwa Facebook kufanya hili sasa au unahizi wamechelewa. Ningependa kusikia kutoka kwako. Tembelea TeknoKona Kila siku kwa habari kede kede za kiteknolojia!.