fbpx

Google Earth yaboreshwa; Sasa picha za Setelaiti ni bora zaidi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Google wametangaza kufanyia maboresho huduma yao ya ramani na picha za setelaiti Google Earth, maboresho hayo yanazifanya picha za setelaiti katika mtandao huu kuwa bora zaidi na zenye taarifa nyingi zaidi ukilinganisha na zile za awali.

Google Earth

Columbia Glacie Alaska, picha kutoka setelaiti mpya

Kwa mujibu wa tangazo lao katika blogu Google wanasema kwamba kuanzia sasa Google Earth itumia picha kutoka katika setelaiti iliyorushwa mwaka 2013 ya Landsat 8. Awali Google walikuwa wanatumia satelite ya Landsat 7 ambayo ilikuwa na uwezo mdogo katika picha na pia ilikuwa inachukua picha chache kwa siku, setelaiti hii mpya inauwezo mkubwa zaidi na pia inapiga picha mara mbili ya idadi ya picha za setelaiti ya kwanza.

INAYOHUSIANA  Google Yamlipa Hacker Wa Urusi Kwa Kugundua Dosari Youtube!

Pamoja na kubadilisha setelaiti pia google wameongeza ubora wa teknolojia yao ya kuhariri picha, hivyo mambo haya mawili yameweza kusaidia picha za sasa kuwa na ubora wa hali ya juu ambao hata kwa macho tu ya kawaida ungeweza kuona tofauti kati ya picha za setelaiti za zamani na za sasa.

Google Earth-New-York-City-Landsat-8-satellite-imagery

Picha mbili za sehemu moja ila ya juu ni kabla ya kufanya mabadiliko na ya pili ni baada ya kuanza kutumia teknolojia mpya.

Kubadilisha setelaiti pia kutaondoa tatizo la picha kuwa na mistari mistari ambalo lilitokana na tatizo la kiufundi katika setelite hiyo ya landsat 7 kuwa limetatuliwa moja kwa moja.

INAYOHUSIANA  Ehang 184; Drone yenye Uwezo wa kubeba Abiria

Lakini yote haya yasingewezekana kama Landsat wasingekuwa na program ambayo inaruhusu watu mbalimbali kutumia data ambazo zimekusanywa na setelaiti zao bila ya gharama wala masharti yoyote.

Endelea kufuatilia mtandao wako wa Teknokona kwa taarifa mbalimbali za Teknolojia katika lugha yako ya kiswahili, kama una swali ama maoni tuandikie katika sehemu ya maoni.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.