fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps iOS Mtandao wa Kijamii Picha Teknolojia Twitter

Twitter: Uwezo wa kupakia picha zenye ubora wa 4K

Twitter: Uwezo wa kupakia picha zenye ubora wa 4K

Spread the love

Twitter ni mtandao wa kijamii kama ilivyo mingine ambayo tunaifahamu na kwa mujibu wa twimu ina zaidi ya watumiaji hai wa kila mwezi zaidi ya mil. 330. Umaarufu huo unaenda sambamba ambapo hivi sasa inawezekana kupakia picha zenye ubora wa 4K.

Kwa muda sasa watumiaji wa Twiitewr wamekuwa wakiweza kupakia picha yenye/zenye ubora wa 2K (2048*2048px) lakini sasa mambo yameboreshwa kote kwa maana ya kwamba Android halikadhalika iOS. Nini maana ya picha yenye ubora wa 4K? Kwa tafsiri yenyepesi kitu ni picha/picha jongefu ukiikuza kwa karibu kabisa zile nukta nukta ndogo sana ambazo zikiungana zinatengeza picha moja zinafikia 4096*4096 kwa urefu na upana.

Ujumbe rasmi kutoka Twitter kuhusu mtumiaji kuweza kupakia picha zenye ubora wa 4K.

Maboresho hayo yameletwa katika mtindo wa aina yake kwani inambidi mtumiaji kwenye kwenye Settings>>Data Usage kisha chagua “On cellular or WiFi” kwa ajili ya kupakia na kuangalia machapisho kwenye Twitter.

kupakia picha

Ukurasa wa mpangilio ndani ya Twitter inayomuwezesha kuweza kupakia, kutaza picha/picha jongefu ya ubora wa 4K.

Habari hii inaweza kuwa imefurahisha wengi lakini maana yake kwa lugha rahisi ni matumizi makubwa ya intaneti kutokana ubora wa kile ambacho utakuwa unataka kukipakia/kukiangalia.

Je, una maoni? Kama jibu ni ndio basi usisite kutu kutuandikia nasi tutajibu kwa haraka iwezekanavyo.

Vyanzo: The Verge, GSMArena

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania