fbpx

Punguza kupokea maombi ya urafiki Facebook

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Facebook inawekana kuwa imekuwa chanzo cha wewe kujuana na watu kutokana na kukutumia maombi ya urafiki na ukakubali, pengine tangu umejiunga Facebook una marafiki 500+.

Kuna wengine wamesharidhika na idadi ya marafiki alionao kwenye Facebook lakini bado anapokea tu maombi ya urafiki kutoka kwa watu mbalimbali na kwa sababu hataki kuongeza idadi hiyo anaamua kutojibu ombi hilo.

Fahamu kuwa kuna njia ya kupunguza ambayo kwa hakika utakuwa unapokea idadi ndogo kabisa au usipokee kabisa kutokana na kigezo kilichowekwa. Ni kitu ambacho hakijajificha ila kinahitaji utundu kidogo kuweza kujua; ingia Settings>>Privacy.

Ukichagua kipengele cha Friends of Friends maana yake ni utapokea ombi la urafiki iwapo tu anyekuomba urafiki ni rafiki wa rafiki yako Facebook.

kupokea

Jinsi ambavyo utapunguza maombi ya urafiki kwenye Facebook.

Ule mtindo wa kupokea maombi ya urafiki mengi kwa siku utapungua/kukoma iwapo utachagua mpangilio huo hapo juu. TeknoKona tumekufahamisha, kazi kwako sasa.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  WhatsApp, Facebook na Instagram zapata shida: Fahamu maeneo yaliyoathirika
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.