Haja ya kujua nini kinaita kwenye simu, hasa kuhusu ujumbe mfupi (SMS) huwa inavuruga kabisa mtiririko na umakini wa kufanya kazi kwenye kompyuta. Kwa kutambua hilo, tumekutafutia ufumbuzi wa tatizo hilo kwa watumiaji wa simu za Androidi, iPhone na windows phone.
Kuna programu kadhaa za kwenye kompyuta na za mtandaoni ambazo bila ya kuzipakia kwenye kompyuta unaweza kutumia ili kutuma na kupokea sms (meseji fupi).
Programu zisizohitaji kupakia kwenye kompyuta (Bila ‘Installation’)
Hizi ni programu za mtandaoni na ni nzuri kama hauna muda wa kupoteza au hauhitaji kuongeza programu nyingine kwenye kompyuta yako ili tu uwe na uwezo wa kutuma meseji.
MightyText, Air Droid na MySms ni programu za mtandaoni kwa ajili ya kutuma na kupokea meseji kwenye simu yako kupitia kompyuta au tableti. Programu hizi zitakuonesha meseji ambazo tayari zipo kwenye simu yako na utaweza kutuma meseji kirahisi kwa kutumia majina ya watu wako kama ulivyozoea kwenye simu yako. Utaweza kujibu sms kirahisi punde zinapoingia na utaweza pia kuona mtu anayekupigia kwenye simu yako ili uamue kuichukua simu na kupokea ama la, kutokana na umuhimu wa mtu utakaeona jina lake.
Kutumia programu hizi za mtandaoni, itakubidi kuishusha mojawapo kwenye simu yako kwanza. Ingia kwenye Google Play store, Windows Store ama Apple iStore na kuishusha kisha, fuata maelekezo ya ku-’sign-in’ kwenye simu yako. Baada ya kuhakikisha inafanya kazi kwenye simu yako, ingia kwenye wavuti MightyText.com/app kama umeweka MighytText ama web.airdroid.com/ kama umeamua kutumia Airdroid au app.mysms.com/ kama umeweka MySMS kwenye simu yako na ufuate maelekezo ya ku-sign-in na hapo pia. Ukifanikiwa kuingia, utaona muonekano mrahisi sana wa kutuma na kupokea ujumbe mfupi wa maandishi – sms.
Zipo programu nyingine lukuki za aina hii kama reachmyphone, desksms na pushbullet ila MightyText, Air Droid pamoja na MySMS ni bora zaidi ukizingatia urahisi wa kutumia na kuaminika.
Programu zinazohitaji kupakia kwenye Kompyuta (Za ku-’install’)
Ingawa muda mwingi unaweza kutumika mwanzoni wakati programu inapakiwa, kutumia programu iliyopakiwa kwenye kompyuta inaokoa muda. Watengenezaji wa simu nyingi zenye majina makubwa kama Samsung, Huawei, Nokia na hata Apple hujipanga kukupa urahisi wa kufanya mambo kadhaa ya simu yako kwenye kompyuta, ikiwemo kutuma meseji. Hivyo basi, itakupendeza zaidi ukijiongezea ujanja kidogo na kuuliza ‘Google’ maswali kadhaa kama ‘ send sms from pc from -simu unayotaka-’.
Samsung hutumia programu yao ya Kies kukupa uwezo wa kutuma meseji ambayo unaweza kuipata kupitia mtandao huu. Huawei nao wana programu ya mtindo kama huo inayokupa chaguzo lukuki za kuimudu simu yako na yaliyomo ikiwa pamoja na kutuma na kupokea meseji ambayo unaweza kuipata kupitia tovuti hii.
Maelezo ya Ziada
Programu hizi za kutuma sms kwa kompyuta zinatumia intaneti kuoanisha (synchronise) akaunti yako ya programu hiyo kwenye kompyuta na programu uliyoweka kwenye simu yako. Kwa mantiki hiyo, meseji ikiingia kwenye simu yako, inasukumwa kwenye akaunti ya programu husika, iwe ni MightyText, Air Droid ama MySms. Ikishaingia huko, utapata taarifa kwenye kompyuta yako kwamba umepata meseji. Ukiijibu kwenye kompyuta, inatumwa tena kwenye simu yako na simu yako inatumia programu ya meseji kwenye simu yako kutuma meseji yako kwa mlengwa. Kama unatumia Mozilla Firefox na Google Chrome, unaweza kupata uwezo na uraisi wa utumiaji zaidi kama utaizipakia au kuweka kumbukumbu (‘Bookmark’) kwenye Vivinjari hivyo.
Ingawa hapa teknokona tunajitahidi sana kurahisisaha maelezo , maelezo haya huenda yasitoshe kwako. Kama kuna mahali haujaelewa jinsi ya kuweza kutuma meseji kwa kompyuta na unataka kufurahia uwezo huu, usisite kuwasiliana nasi teknokonatz@gmail.com pamoja na kurasa zetu za facebook na twitter pamoja na instagram.
Picha Na:
No Comment! Be the first one.