App ya ramani katika vifaa vya Apple inajulikana kama Maps imetimiza miaka kumi tangia kuanzishwa kwake.
Kama ni mtumiaji wa iPhone ni wazi kuwa umeshwahi kuiona App hii ya Maps katika simu yako, ni wazi kuwa huduma hii imebadilika sana tangia kuanzishwa kwake.

Kizuri pia katika App hii ni kwamba kama utakua kwenye majiji makubwa ambayo ni maarufu sana hata uonekanaji wake ndani ya App ni wa aina yake.

Vitambulisho kama madaraja maarufu, sanamu maarufu n.k katika miji kwa kupitia App hii vinaweza kuonekana kwa urahisi zaidi, jambo ambalo hapo awali halikuwezekana.
Kinginie kizuri ni kwamba unaweza ukabadilisha aina ya jinsi unavyoona ramani, unaweza kuweka iwe inaonyesha mfumo wa satelaiti (mfumo wa mbali zaidi).

Uwezo wa 3D ambao huu ni uwezo wa kuonyesha picha halisia kwa kiasi kikubwa sana, yaani barabara na vitu vinavyozunguka katika mazingira Fulani vitaweza kuonekana vizuri zaidi.
Chanzo: The Verge
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je unachukuliaje mwendelezo huu na ukuaji wa App hiyo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.