Jarida moja la nchini Korea Kusini limechapisha ripoti juu ya simu mpya ya Samsung Galaxy S7, pamoja na kuelezea tarehe inayotegemewa kuingizwa sokoni, inasemekana kwamba simu hii itatolewa kwa awamu mbili tofauti.
Ripoti hii iliyochapishwa na mtandao wa Korea Kusini wa ET inasema kwamba Samsung watazindua simu yao mpya ya S7 kwa matoleo mawili (kama vile ambavyo mahasimu wao wa Apple wamekuwa wakifanya kwa bidhaa zao). Matoleo mawili ya S7 ni pamoja na lile lenye kioo cha inch 5.2 na ile yenye kioo cha nchi 5.5 (hii itakuwa curved). Hii ni mara ya kwanza Samsung kutoa simu katika matoleo mawili tofauti ambayo yana vioo vya ukubwa tofauti, Apple ndio wamekuwa wanatumia huu mtindo kutoa simu zao.
Pia ripoti hii imesema kwamba Samsung wanatatengeneza simu milioni 3.3 kwa S7 yenye kioo cha kawaida na takribani simu milion 1.6 kwa ile yenye kioo kilicho kuwa curved (ambayo imepewa jina la Galaxy S7 Edge) hii itafanya simu zitakazotengenezwa kwa awamu ya kwanza itakuwa ni takribani milioni 5.
Tofauti na tetesi za mwanzo kwamba S7 ingekuja na matoleo manne tofauti tofauti ripoti hii imesema kwamba kutakuwa na matoleo mawili tuu ambayo yatatoka kwa mfumo kama ule unaofanana na mfumo unaotumika na Apple.
Msemaji wa Samsung alipoulizwa kuhusu ripoti hii alikataa kusema chochote juu ya ripoti hii ambayo imesambaa katika mitandao mingi ulimwenguni.
Hii ripoti haijasema chochote kuhusu bei ya simu hii hivyo bado tunategemea kwamba tetesi za kwamba simu hii itauzwa kwa bei chee soma hapa bado hazijathibitishwa ingawa zimekuwapo ripoti kwamba kwa sababu hii simu itakuwa na Iris scanner basi bei yake itakuwa ghali ukilinganisha na Galaxy S6.
lakini hizi ni tetesi na hazijathibitishwa
Zaidi ripoti hii inaonesha kwamba utengenezaji wa simu hii kwa wingi utafanyika wezi wa pili mwakani na pia inategemewa itazinduliwa kipindi hicho hicho.
Endelea kuwa nasi ili kuzipata taarifa za kiteknolojia katika lugha yetu ya Kiswahili kwa wakati.
No Comment! Be the first one.