Siku hizi teknolojia imekua sana hivyo ni vigumu kuuza kitu chochote mtandaoni na kupata kile unachostahili. Watu wengi wanapakua vitu bure na kiwizi wizi katika mitandao hii. Kitendo hicho kinajulikana kama Uharamiaji (kwa kimombo piracy).
Muvi,miziki, magemu kama GTA V na mafaili mengine mengi yanapatikana katika mitandao kwa njii hii ya uharamizi. Wengi haswa wale wenye haki miliki wanapinga kitendo hiki lakini watumiaji wengi wa mwisho ndio imekua kimbilio lao. Fikiria unaweka kazi yako vizuri katika mtandao ili uuze lakini anatokea mtu nae anaweka kopi ya kazi hiyo hiyo katika mtandao tena bure kabisa
Tafiti zimefanyika ili kubaini ni gemu gani limeshishwa kinyemela mara nyingi kuliko yote. Gemu la maisha ya kihuni ya Grand Theft Auto 5 (GTA V) ndio limeshika usukani baada ya kuonekana kuwa ndio limeshushwa sana kuliko magemu mengine katika mtandao tena kuwa njia ya uharamizi.
Tafiti zilifanywa na kampuni la BitSight, na hii ni moja tuu kati ya taarifa ambazo zilifanywa na kampuni hiyo
Ukiachana na GTA V pia Adobe Photoshop na yenyewe ilikua miongoni mwa zile zinazoongoza kushushwa na watu kinyemela katika mtandao.
Ripoti ilikuta kuwa asilimia 39 ya magemu yaliyoshushwa kwa kutumia ‘torrents’ mbalimbali na App zingine kwa asilimia 43 zilizoshushwa kutoka mitandao mbalimbali ya kiharamizi huwa vyote vinaingia katika kompyuta na baadhi ya mafaili ambayo ni hatarishi kwa kompyuta
Na hii inatokea hata kwa watu wa ofisini kwani huwa wanatumia sasa intaneti hiyo ya bure (ya ofisi) sasa hapa madhara yake ni kwamba mtu anaweza ambukiza kompyuta zingine za ofisini kutokana na kile kitu alichokishusha kinyemela kutoka mtandaoni bila hata ya yeye kujua.
Je kwa nini watu wanafanya hivyo? Wengine hupendelea kushusha kwa njia hizi rasmi kwa nia ya kujaribu magemu au programu husika, na kama wamependa ndio wananunua katika njia rasmi. Pia wengine hushusha kwa njia hizi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kipesa wa kununua.
Ukiachana na GTA V katika upande wa magemu hata magemu kama The Sims 4, Mortal Kombat X, FIFA 15 na The Witcher yalionekana kuwa miongoni mwa yale yanayoshushwa sana kutumia mitandao hii ya kinyemela.
Katika programu zinazoongozwa ukiachana na Adobe photoshop kuna Microsoft Office, ikifuatiwa na programu endeshaji za Microsoft Windows 8.1, Microsoft Windows 7 na Microsoft Windows 10.
No Comment! Be the first one.