fbpx
Tanzania, Teknolojia

Kadi janja kwa ajili ya Usafiri wa Mabasi ya Mwendo Kasi zaanza Kuuzwa

kadi-janja-kwa-ajili-ya-usafiri-wa-mabasi-ya-mwendo-kasi
Sambaza

Kwa watu waliokweishatumia usafiri wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam basi wanajua moja ya changamoto kubwa iliyokuwepo ni ukataji wa tiketi. Kadi janja kwa ajili ya usafiri wa mabasi hayo zaanza kupatikana.

Kadi janja kwa ajili ya Usafiri wa Mabasi

Kadi janja hizo (Smart cards) zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza foleni za ununuaji tiketi kila pale unapotaka kutumia usafiri huo. Kupitia kadi hiyo utaweza kuweka salio la kati ya Tsh 5,000 hadi Tsh 30,000 na kisha utakuwa unakatwa kwa kila safari utakayokuwa unasafiri katika huduma hiyo ya mabasi ya mwendo kasi.

INAYOHUSIANA  CES 2016: LG Kuonesha Kioo (screen) Chao cha Kukunja

Kampuni ya Maxicom ndio inayosimamia teknolojia hiyo. Utaweza kupata kadi janja hiyo kwa sh 5,000 na Tsh 4,500 inaingizwa moja kwa moja kwenye kadi hiyo tayari kwa kuanza kutumika katika kulipia safari na hivyo kufanya gharama ya kadi hiyo kuwa ni Tsh 500 tuu.

Kuweka pesa katika kadi hiyo kutaweza kufanyika kupitia huduma za malipo ya simu, vituo vya Max Malipo na ata kwenye vituo vya mabasi hayo.

INAYOHUSIANA  Kipindi hichi cha Covid-19, Roboti wa kuchukua ajira za watu wapata umaarufu zaidi

Kurahisha mambo, ndio moja ya faida kubwa ya teknolojia! Usisahau kuungana nasi kupitia Twitter, Facebook na Instagram

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |