fbpx
Tanzania, Teknolojia

Tanzania yaongeza ulinzi wa teknolojia kwa wanyama pori

tanzania-yaongeza-ulinzi-wa-teknolojia-kwa-wanyama-pori
Sambaza

Mataifa mengi duniani kila mara yanajitahidi kutumia mbinu za kisasa zaidi ili kuwezesha kulinda wanyama pori ambao wapo kwenye hatari ya kutoweka kutokana na vitu ambavyo wanavyo na vyenye thamani kubwa kutokana na kuuzwa kimagendo.

Katika miaka ya karibuni na iwapo wewe ni kati ya wale wanaopenda kufanya utalii wa ndani sio kitu cha ajabu kusikia suwa siku hizi mbuga zatu hifadhi za wanyama pori zinalindwa kwa vifaa vya kidijiti kama vile kamera zilizofungwa kwenye ndege zisizotumia rubani. Hii inatoana na uwindaji haramu uliokithiri ambao unatishia kutoweka kwa wanyama fulani fulani porini.

Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeweka wazi kuwa upo mpango wa kutumia kifaa cha kijeografia (GPS-Global Positioning System) kulinda Tembo kufuatilia, kuzuia ujangili na kuvutia watalii zaidi.

Vifaa hiyo vya kijeografia vitakuwa vianafuatilia mienendo yao na hata kupunguza kama sio kumaliza matukio ya Tembo kuvamia mashamba. Mbali na hilo, patawekwa uzio jambo ambalo litasaidia kukabiliana na majangiri (uwindaji haramu).

wanyama pori
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Khamis Kigangwala akindindua mpango wa kulinda Tembo kwa kifaa cha kijeografia.

Mradio huo umedhaminiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF) kwa kiasi cha $300,000|Tsh. 800 milioni ambapo mpaka sasa Tembo wapatao tisini na watano (95) walio kwenye hifadhi mbalimbali nchini Tanzania wamefungwa vifaa hivyo.

Vyanzo: Gazeti la Mwananchi, Global Publishers

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Fahamu kuhusu Ninogeshe na HaloPesa
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|