Kompyuta za Chromebook zinatengenezwa na Google na kimsingi hazivumi sana kiasi cha kujulikana na wengi kiasi cha kuwa maarufu lakini ukweli ni kwamba zipo!.
Opera Mini ni kivinjari ambacho kinafahamika na wengi tuu kutokana na yale mengi ambayo yamewekwa kwenye kiwezeshi hicho cha kuperuzi mtandaoni na kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni kwenda kwao kwenye Chromebook kunakifanya kuwa kivinjari cha kwanza kilichonyumbuliwa kuweza kufanya kazi bila tatizo.
Kwanini Opera Mini ndio kivinjari “Cha kwanza” kwenye Chromebook mpya?
Ndani ya toleo jipya la kompyuta za Chromebook kipo pia kivinjari cha Mozilla Firefox lakini kikipatikana katika muundo wa ilvyo kwenye simu. Sasa sababu ya Opera Mini kuwa kivinjari cha kwanza inatokana na kuwa katika muundo wa Android lakini kuweza kutumika vizuri kabisa kwenye kompyuta na kwenda sambamba kabisa ilivyo komyuta tofauti na mambo yalivyo kwenye Firefox ndani ya toleo jipya la Chromebook.
Kama kawaida zile sifa za kivinjari hiki kama upatikanaji wa Messenger ya ndani kwa ndani, uwezo wa kuzuia matangazo, uwezekano wa kutengeneza mtandao wako mwenyewe (VPN), mfuko wa kuhifadhi sarafu za kidijiti pamoja na sifa nyingine za kuihusu zinapatikana ndani ya kivinjari hicho kwenye kompyuta za Chromebook toleo jipya.
Si ajabu kwa Opera Mini kutokuwa maarufu kwa watumiaji wengi lakini kwa ambao wanajua raha ya kutumia kivinjari hicho; kutumia kingine unahisi kama kuna kitu umepungukiwa au sio?
Vyanzo: Gadgets 360, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.