fbpx
Oppo, simu, Teknolojia, Uchambuzi

Simu ya Oppo F11 Pro toleo la pili! #Uchambuzi

oppo-f11-pro-toleo-la-pili
Sambaza

Imepita miezi miwili sasa tangu toleo la kwanza la simu janja kutoka Oppo kutoka lakini karibu miezi miwili baadae kampuni huika imeona inafaa kutoa simu janja nyingine ama kwa lugha rahisi Oppo F11 Pro toleo la pili.

Nianze kwa kuuliza ni ukubwa gani wa diski uhifadhi unapenda simu janja utakayonunua iwe nayo? Wakati unafikiria jibu fahamu ya kuwa Oppo wametoa toleo la pili kwa simu janja ambayo imetofautiana sehemu moja tu na ile ya nyuma yake; upande wa memori ya ndani ya kwanza lile toleo la kwanza ina GB 64 halafu hii ya pili ina GB 128.

INAYOHUSIANA  Kwa Kushangaza Kabisa, Pengine Hii Ndio Simu Ya Mwisho Ya Microsoft Inayotumia Jina La Nokia!

Je, sifa nyinginezo ni zipi?

Kipuri mama/kioo. Simu hiyo toleo la kwanza na pili zote zimezinduliwa nchini India, rununu uhusika ina Mediatek Helio P70 SoC, kioo cha LCD kina urefu wa inchi 6.53.

RAM. Katika miaka ya karibuni makampuni mengi yameongeza nguvu kwenye RAM kutoka GB 2-3 hadi GB 6 kama ilivyo kwa Oppo F11 Pro.

Kamera. Toleo la pili (F11 Pro) linalobeba jina la Oppo lina kamera mbele iliyowekwa kitofauti; nyuma ina kamera mbili-MP 48+MP 5 halafu ile ya mbele yenye uwezo wa “Kujitokeza na kujificha” ina MP 16.

INAYOHUSIANA  Mapya kutoka Apple: MacBook Air 2018 na Mac Mini mpya
Oppo F11 Pro
Oppo F11 Pro toleo la pili lenye GB 128.

Uwezo wa betri/Mengineyo. Hapa unakutana na betri amabyo ina mAh 4000 lakni pia kama kawaida kuna teknolojia ya kuchaji haraka. Rangi zake ni Nyeusi na Bluu, imewekwa Android Pie, teknolojia ya alama ya idole ipo kwa nyuma kama kawaida, tofauti ya bei kati ya toleo la GB 64 na GB 128 ni $14 tu (64GB ni $358).

Kupitia Amazon simu hiyo inauzwa kwa $372|zaidi ya Tsh. 855,600. Sasa wewe ndio utafanya maamuzi endapo utapenda kununua toleo la kwanza au la pili.

Vyanzo: Gadgets 360, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|