fbpx

Uber yaingia kwenye ulingo wa kumilikiwa na wengi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

kampuni inayojihusisha na biashara ya usafirishaji wa kukodi lakini “Haimiliki vyombo hivyo vya usafiri” sasa imeona iungue ukurasa mpya kwa kuingia kwenye ulingo wa kumilikiwa na wengi.

Uber kampuni inayofanya shughuli zake nchi nyingi duniani na kutokea kurahisisha uaptikanaji wa usafiri wa kukodi imeingia kwenye kumbukumbu kwa kuamua kuiweka kampuni hiyo kwenye soko la hisa kuanzia leo (Mei 10 2019) baada ya kuanzishwa kwake muongo mmoja (miaka 10) uliopita. Sasa tafsiri yake ni kwamba kampuni hiyo imeanza kumilikiwa na wengi.

Uber ni kampuni ya wapi na ya nani? (Historia fupi ya UBER)

Hii ni kampuni ya usafirishaji wa kukodi ilyoanzishwa mwaka 2009 na Travis KalanickGarrett Camp huko San Franscico Marekani ingawa kwa sasa ina makao makuu San Francisco na California Marekani. Uber inatoa huduma mbalimbali zikiwemo kuchangia usafiri na mtu mwingine (ikiwemo baiskeli) na kuletewa chakula.

Uber imewekwa kwenye soko la hisa la New York (NYSE) na bei ya hisa ikawa ni $45, ikashuka hadi $42 na kumaliza siku (soko la hisa kufungwa) ikiwa ni $41.57 kwa hisa moja. Katika siku ya kwanza ndani ya soko la hisa mambo hayakwenda vizuri kwani bei ilionekana kushuka badala ya kupanda tofauti na matarajio ya wengi ambao walitegemea angalau kwa siku hii ya kwanza bei yake ingepanda na badaala yake ikaishia kuuzwa $41.57/hisa moja.

kumilikiwa na wengi

Uber yaingia kwenye umiliki wa wengi.

UBER inatoa huduma kwa kumuita dereva aliyesajiliwa na kampuni hiyo kwenye nchi husika kupitia programu tumishi na huduma hiyo inapikana katika maeneo 785 duniani kote.

UBER wamefuata nyayo za kamapuni mengine makubwa kama Facebook ambayo iliingia kwenye soko la hisa mwaka 2011. Sasa hata na wewe unaweza ukawa mmoja wa wamiliki wa kampuni husika 😆 😆 .

Vyanzo: Business Insider, TechCrunch

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Kuhamisha App Na Taarifa Zingine Kutoka Simu Moja Kwenda Nyingine!
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.