Kuna mtu anakwambia umri wa mtu ni kigezo cha mtu huyo kujifunza mambo ya kidigitali? Mwambia hayupo sahihi, bibi kizee wa miaka 81 azindua app kwa ajili ya watumiaji wa iOS/iPhone.
 

Bibi huyu mwenye jina la Masako Wakamiya wa nchini Japani alianza kutumia kompyuta kwa mara ya kwanza takribani miaka 21 iliyopita, akiwa na umri wa miaka 60. Kuhusu suala la kazi ingawa sasa hivi ni mstaafu ila ameshawahi kufanya kazi benki kwa muda wa miaka 43.
App yake yenye jina la Hinadan, ametengenezwa kwa ajili ya wajapani kama sehemu ya kuizimisha utamaduni wa nchini humo ujulikanao kama Hinamatsuri (yaani Girls’ Day – Siku ya wadada). App hiyo ingawa ni kama gemu lengo kuu lake ni kuwafundisha watu jinsi ya kupangilia midoli yao mbalimbali sahihi kwenye maonesho ambayo huwa yanafanyika katika maadhimisho ya utamaduni wa Girls’ Day.
Mtu anakuwa anashinda katika gemu hilo kama akifanikiwa kuipanga midoli hiyo kwa usahihi kabisa.


Bibi huyo hajafanikiwa katika hili tuu kwenye eneo la masuala ya kidigitali, bali anamiliki pia blogu ambazo anaandika kwa lugha ya kijapani na kiingereza ambapo huwa anazungumzia masuala ya ubunifu kwa kutumia programu ya Excel na pia huwa anazungumzia safari mbalimbali za matembezi ambazo huwa anafanya.
Unaweza pakua app yako kutoka soko la App Store – iTunes/iOS