fbpx
Betri, Teknolojia

Betri kubwa duniani yazinduliwa; Musk atimiza ahadi yake

betri-kubwa-duniani-yazinduliwa

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa makala zetu basi utakumbuka miezi kadhaa iliyopita tuliandika kuhusu betri kubwa duniani kutoka Tesla ilikuwa imekamilika kwa asilimia 50. Sasa si 50% tena bali ni kwa asilimia 100 na tayari imeshaanza kufanya kazi.

Bilionea aliyewekeza zaidi kwenye biashara ya vifaa vya kieletroniki, Elon Musk ametimiza ahadi yake ya kukamilisha ujenzi wa betri kubwa kabisa duniani ambayo imetengenezwa na Tesla kukamilika katika siku 100. Bw. Musk ahadi hiyo ameitimiza na tayari betri hilo limezinduliwa na kuanza kufanya kazi huko nchini Australia.

Kutokana na kimbunga kilichotokea mwaka 2016 huko Australia na kusababosha eneo la Kusini mwa Australia kuwa gizani kabisa (kutokuwa na umeme) ndio kilichomsukuma Bw. Musk kujenga betri kubwa ulimwenguni kutatua tatizo hilo la upungufu wa umeme.

Betri kubwa kuliko zote duniani inayotumika kuzalisha nishati ya umeme nchini Australia.

Sifa za betri kubwa kabisa ulimwenguni kutoka Tesla.

Betri hiyo ina nguvu kiasi cha 100 MW/129 MWh iliyoopo Jamestown Kask mwa Adelaide. Betri hiyo hivi sasa inatoa huduma ya umeme wa uhakika kwa nyumba zaidi ya 30 elfu kwa saa 24 kila siku. Hivi sasa Australia ndio nchi inayoongoza ulimwenguni kwa kuwa chanzo cha uhakika cha kuzalisha umeme mbadala saa 24/7.

INAYOHUSIANA  Duo yapelekwa kwenye tabiti na iPad

Katika siku ya kwanza tu betri hiyo iliweza kuzalisha kiasi cha 70MW kilichotumika kuzungusha mashine za kuzalisha umeme wa nishati ya upepo.

Muonekano wa juu wa betri kubwa zaidi duniani.

Betri hiyo inatarajiwa kusaidia kwa kuzalisha umeme wa uhakika na kitu ambacho ktapunguza upungufu wa umeme Kusini mwa Australia. Mradi wa ujenzi wa betri hilo kubwa zaidi duniani unakadiriwa kumgharimu Elon Musk $50 milioni.

Ambacho wengi hawakifahamu kuhusu Ausralia.

Australia ni moja ya wazalishaji wakubwa wa makaa ya mawe. Zaidi ya 60% ya nishati inayozalishwa nchini humo inaotokana na makaa ya mawe, 14% ya makaa ya mawe inatoka kwenye vyanzo mbadala.

Nchini Australia kipindi hiki ni cha Jua kali hivyo kukamilika na kuanza kutumika kwa betri hiyo kumeleta faraja kwa wananchi wengi waopata umeme unaozalishwa kutokana na nguvu ya betri hiyo yenye sifa ya kipekee kwa kuwa betri kubwa zaidi duniani.

Vyanzo: Telegraph, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|