fbpx

Kuhusu kutuma taarifa za kisimbuzi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Tunakumbuka vyema kuhusu sakata la kuhusu kuonyesha chaneli za ndani bila ya malipo na baadhi yetu naamini bado hatupati huduma hiyo mpaka sasa lakini tukaambiwa tutume taarifa za kisimbuzi unachotumia kati ya AZAM, DSTV au ZUKU.

Katika hali ya kiubinadamu unaweza ukawa ni mmojawapo ya watu ambao wamejisahau kutuma taarifa za king’amuzi vilivyotajwa kwenye utangulizi na ni vyema ukafahamu kuwa tarehe ya mwisho ya kutuma taarifa hizo inakaribia!.

Mwisho wa kutuma vitu vilivyoainishwa kwenye jedwali lifuatalo ni Septemba 24 2018.

taarifa za kisimbuzi

Tangazo linalohusu kutuma taarifa za kisimbuzi kwenda TCRA.

Mambo yawekwa kijitali (unaweza ukatuma kwa barua pepe) njia ambayo kwa maoni yangu naona itakuwa ni rahisi kuliko kutuma kwa njia ya Posta. Sasa ni wewe mwenyewe itakubudu utumie njia itakayokuwa rahisi kwako.

INAYOHUSIANA  Simu imepotea tuma IMEI kwenda cop@vsl.net - Hii habari ni ya uongo, usifanye hivyo

Inawezekana ukawa umekata tamaa kuhusu hatima ya wewe kupata tena huduma ya kutazama chaneli za ndani lakini kuitikia ombi si jambo baya.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.