fbpx

Samsung watoa Galaxy A7 2018

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Samsung ambao wamekuwa wakifanya vizuri kwenye soko la ushindani bado wameendelea kutoa simu janja na kwa mwaka huu wana rununu ya kwanza ambayo ina kamera tatu nyuma, inaitwa Galaxy A7 2018.

Simu hiyo inaonekana kuwa nzuri na ya kuvutia kwa sababu mbalimbali lakini kubwa ni kuwa na kamera ambazo lenzi yake inatoa picha ambazo ni ang’avu bila kusahau kutokuwa ghali.

Galaxy A7 2018

Kamera tatu za kwenye Galaxy A7 2018.

Sifa za  Galaxy A7 ya mwaka 2018.

Kipengele

Maelezo

Kipuri mama/Uwezo wake Jina la prosesa iliyowekwa huko haijafahamika ingawa kasi yake ni 2.2GHz.
Kioo Kioo kina urefu wa inchi 6, rangi za ubora wa hali ya juu (FHD+ Super AMOLED) na kiujumla simu yenyewe ina uzito wa gramu 168.
Kamera Upande wa nyuma: Zipo tatu; yenye MP 5, MP 24 na MP 8.

Kwa mbele: Ipo moja tu na ina MP 24.

RAM/Memori ya ndani RAM GB 4 au 6 na diski uhifadhi ni GB 64/128 huku ikwa na uwezo wa kuweka memori ya nje mpaka GB 256
Betri/Programu endeshi 3300mAh ndio nguvu ya betri yake ikiwa na Android 8 (Oreo) upande wa programu endeshi.
Mengineyo Rangi: Bluu, Nyeusi, Dhahabu na Udhurungi.

Mawasiliano: 4G VoLTE.

Pia ina Bluetooth v5.0, ANT+, NFC, GPS, GLONASS, Beidou na sehemu ya kuchomeka spika za masikioni ukubwa wa 3.5mm.

INAYOHUSIANA  CES 2016: LG Kuonesha Kioo (screen) Chao cha Kukunja

Galaxy A7 2018 inatazamiwa kuanza kupatikana duniani kote katika siku za usoni na bei ya ughaibuni ni $410|Tsh. 943,000.

Vyanzo: Gadgets 360, Engadget

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.