Mara nyingi tunashindwa kusnapchat baadhi ya matukio katika mtandao wa kijamii wa Snapchat kwasababu tu katika kundi la marafiki kuna mtu hautaki aone unachopost.
Ukweli ni kwamba sio lazima kila rafiki yako aone video na picha zako unaweza kuamua katika marafiki zako ni nani na nani wawe wanaona yale unayopost.
Makala hii itakusaidia kujua namna ya kuchagua katika marafiki zako ni wapi waweze kuona yale ambayo unayaweka katika Snapchat.
- Fungua Snapchat kisha gusa ki-ghost cheupe ambacho kipo juu katika ya ukurasa mkuu wa snapchat ambao unapatikana ukifungua tu app yako.
- Gusa alama ya mpangilio (settings) kisha ingia katika eneo la mpangilio, Hapo utaona sehemu imeandikwa Who can …ambayo ndiyo inatumika katika kufanya mipangilio ya faragha.
- Katika sehemu hii utaweza kuona sehemu mbili moja ni who can contact me na ya pili ni who can view my story.
- Nenda katika who can view my story na hapa utakutana na machaguo matatu Everyone, My Friends na Custom katika haya machaguo matatu kama unataka baadhi ya watu tu ndio wawezae kuona unavyopost katika snapchat basi chagua Custom
- Katika Custom basi hapa utaletewa orodha ya marafiki wako na wewe utachagua ni wapi wanaruhusiwa kuangalia yale unayopost na wapi wasiruhusiwe.