TCRA ilifanya uchunguzi wa ubora wa huduma ambazo zinatolewa na mitandao ya simu ya TIGO HALOTEL VODACOM AIRTEL SMART pamoja na ZANTEL, katika uchunguzi huu uliofanyika mwezi Februari na Machi katika miji ya Dar es salaam Arusha na Mwanza ulipima kila mtandao katika vigezo mbalimbali tisa.
Katika makala hii uchambuzi wangu unajikita katika vigezo vitatu tu katika vile ambavyo TCRA iliviangalia katika uchunguzi wake pia uchambuzi wangu umeangalia matokeo ya 3G pekee ingawa uchambuzi wa mamlaka ulihusisha pia 2G, vigezo ambavyo makala hii itachambua ni Simu kushindwa kuunganishwa, Simu kushindwa kumalizika (yaani kukatika njiani) na Ubora wa sauti katika simu hivi ni vipengele ambavyo mitandao yote ilipimwa.
> Dar es salaam
Mtandao wa TIGO ndio kinara kwa kuwa na kiasi cha simu chache zilizoshindwa kuunganishwa huku mitandao mingine yote ikishindwa kufaulu jaribio hilo, kwa upande wa simu kushindwa kumalizika mtandao wa TIGO ndio ulikua na simu chache zaidi zilizoshindwa kumalizika ukifuatiwa na VODACOM na HALOTEL. Kwa upande wa jaribio la ubora wa sauti mtandao wa AIRTEL ndio ulio ongoza na ukifuatiwa na HALOTEL pamoja na VODACOM kama inavyoonekana katika grafu hapo chini.
> Mwanza
Kwa mujibu wa majaribio yaliyofanywa na TCRA ni VODACOM pekee ndio walifaulu kigezo cha simu kushindwa kuunganishwa kwa sababu mitandao mingine ilipata idadi kubwa ya simu kushindwa kuunganishwa kuliko idadi inayotakiwa na TCRA, kwa upande wa simu kushindwa kumalizika (yaani simu ambazo zinakatika katikati ya maongezi) VODACOM TIGO na HALOTEL ndio walio ibuka vinara baada kuwa na simu chache ambazo zilikatika katikati ya mazungumzo kama ambavyo grafu inaonesha. Katika upande wa ubora wa sauti katika mtandao wa 3G hakuna mtandao ambao ulifikia viwango vilivyowekwa na TCRA.
> Arusha
TCRA inasema kama unaangalia mtandao ambao hauna matatizo ya simu kushindwa kuunganisha katika 3G kwa Arusha HALOTEL ndio imefikia viwango mitandao mingine haikufikia viwango vilivyowekwa na TCRA, na kama unaaangalia mtandao ambao hautakuwa na uwezekano wa simu kukatika katika hovyo basi HALOTEL SMART, TIGO na VODACOM ndiyo mitandao ambayo unaitafuta kwa sababu AIRTEL wao hawakufaulu kiwango kilichowekwa na TCRA. Na kama unatafuta mtandao wenye ubora wa sauti wakati wa maongezi basi SMART ndiyo mtandao pekee uliokidhi vigezo vya TCRA kwa mtandao wa 3G Arusha.
One Comment
Comments are closed.