Facebook Messenger leo imefanya mabadiliko makubwa katika app zake katika upande wa emoji kwa kuzifanyia mabadiliko makubwa emoji hizi pamoja na kuongeza emoji nyingine mpya.
Mabadiliko haya yatawafanya watumiaji wa app hii katika Android na wale wa iOS kutumia emoji za aina moja hivyo kuwaleta karibu zaidi.
Facebook Messenger wanasema kwamba pamoja na mabadiliko haya kuondoa mkanganyiko uliokuwa unatokea watu wa kutoka OS tofauti wanapotumiana emoji pia yanawapa shavu zaidi wanawake baada ya kuhakikisha kwamba wanapata uwakilishi mkubwa katika emoji.
Nini Kipya!?
Facebook Messenger imeleta kwanza uwezo wa kubadili rangi ya ngozi ya emoji unayotumia, pia imeleta emoji nyingi ambazo zinawakilisha wanawake katika kazi mbalimbali za kitaaluma kama vile askari wa kike zaidi wanawake wamewakilishwa katika emoji ambazo walikuwa hawawakilishwi kama vile mtu anayekimbia na kutembea.
Mabadiliko haya yataanza kupatikana lini kwa watumiaji?
Facebook Messenger inaanza kuyatoa mabadiliko haya leo siku ya alhamisi lakini sio kwa wateja wote kwa pamoja, wapo ambao wataipata mapema zaidi ila wengine watasubiri zaidi. Ili kupata mabadiliko haya basi itakubidi kuupdate app yako pindi mabadiliko haya yatakapokufikia.