Kuongezeka kwa watumiaji simu janja (smartphones) kunazidi kuchangia ukuaji mkubwa wa utumiaji huduma za intaneti na hivyo kuzidi kukuza wastani wa utumiaji data kwa mwezi duniani kote.
Kati ya robo ya kwanza (Q1) ya mwaka 2015 hadi robo ya kwanza ya mwaka huu (2016) utumiaji wa data umekuwa kwa zaidi ya asilimia 60 duniani kote. Hii inamaanisha usafirishaji wa data kupitia huduma ya intaneti unaochangiwa na utumiaji wa huduma mbalimbali unazidi kuongezeka.
Katika ripoti iliyotolewa na shirika nguli la vifaa vya mawasiliano la Ericsson, imeonekana ukuaji huo unaendelea na hauna dalili wa kupunguza kasi.
Katika kipindi cha miezi mitatu (Q1) ya mwanzo kwa mwaka 2016 kulikuwa na kiasi cha data cha Exabyte 5.7 kilichotumika na huduma za video, mitandao ya kijamii na muziki ndizo zilizochangia zaidi.
GB 1000 = 1TB, halafu TB 1000 = 1PB (Perabyte), halafu PB 1,000 ndio sawa sawa na Exabyte 1
Ukubwa wa diski uhifadhi unaanzia – MB (Megabyte) -> Gigabyte (GB) -> Terabyte (TB) -> Petabyte (PB) -> Exabyte (EB) -> Zettabyte (ZB)
Asilimia kubwa ya utumiaji wa data huu unatokana na watumiaji wa simu janja. Mitandao ya simu ina changamoto kubwa katika kuwekeza zaidi katika mitambo yake kwani miaka kadhaa nyuma utumiaji wa huduma za intaneti na jumla ya data iliyokuwa inasafirishwa kwenye mitambo yao haikuwa kubwa kiasi hichi.
Wastani wa utumiaji data kwa kila simu janja bado upo chini katika mataifa ya Afrika wakati upo juu sana katika bara la Amerika Kaskazini. Wakati Afrika na Asia wastani ukiwa chini ya GB 2 huko Amerika Kaskazini wastani ni takribani GB 4 kwa kila mtumiaji simu janja.
Je wewe unatumia kiasi gani cha data kwa mwezi? GB 2, 4, 5, 10, ……?
[socialpoll id=”2364417″]
Chanzo: Ericsson