fbpx

Uhalifu wa mitandaoni unazidi kudhibitiwa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

vodacom swahili

Sambaza

Watu 21 wamekamatwa kwa kuwalaghai maelfu ya watu kupitia mitandaoni na kuwaibia kiasi kikubwa cha fedha nchini Uchina.

Kwa mujibu wa shirika la Sinhua, watu zaidi ya 20 chini ya jina la jukwaa la uwekezaji wa intaneti, walidanganya watu kwa kuwaahidi kuwa watapata kipato zaidi. Watu hao 21 wamejipatia kipato kinyume na sheria cha takribani $132 milioni kupitia mtandaoni.

Watuhumiwa wametajwa kuwa na umri kati ya miaka 16 na 20 wamekuwa wakiiba fedha za watu kupitia katika tovuti za manunuzi ya mitandaoni na imebainika wamefanya uhalifu kwenye takribani majimbo 12 ya Uchina.

Imeelezwa kuwa polisi wa Uchina walianza ufuatiliaji wa kiufundi na kuweza kubaini jukwaa la ulaghai mwezi Desemba 2017. Baada ya miezi 6 ya ufuatiliaji wa kiufundi uliofanyika  Guangdong, Ciangshi, Ciciang na Guangxi Cuang watu hao 21 wamepatikana na kukamatwa.

Taarifa haijaweka wazi ni tovuti gani hasa iliyotumika kuwaibia watu lakini imebainika kuwa tovuti waliyokuwa wanaitumia ilikuwa katika mji wa Linyi ulioko katika jimbo la Shandong Mashariki mwa Uchina na iliweza kuchukua saa 2 na nusu kwa mtu kuweza kuibiwa kiasi cha fedha katika akaunti yake.

Uhalifu wa mitandaoni

Watu wanaoibiwa ni wale ambao akaunti zao wamezisajili kwa ajili ya manunuzi ya mtandaoni na hawakutunza vizuri taarifa za akaunti zao.

Baada ya uchunguzi wa muda wa miezi mitatu polisi walifanikiwa kurudisha kiasi cha Yuan 800,000 (zaidi ya Tsh. 266m) kilichoibwa kutoka kwa watu kupitia benki mbalimbali.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Nunua Bidhaa Instagram: Instagram wanakuja na huduma ya manunuzi
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.