fbpx

Samsung kuzindua memori kadi ya 512GB

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kampuni ya Samsung imetangaza hivi karibuni itajiunga na orodha ya makampuni machache ambayo yamezindua memori kadi (microSD) yenye ukubwa wa 512GB.

Mpango wa kuzindua memori kadi yake ya ukubwa huo umesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa masoko, Drew Blackard wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya Samsung galaxy Note 9.

Ingawa simu nyingi za kisasa zinaruhusu kuweka memori za ukubwa wa 512GB mpaka 1TB lakini ukweli memori kadi za ukubwa huo zipo chache mno kwa sasa katika soko.

memori kadi ya 512GB

Memori kadi za ukubwa wa 256GB ndio zinapatikana kwa wingi katika soko tofauti na memori kadi za ukubwa wa 512GB zinazotengenezwa na kampuni chache.

Ujio wa memori kadi hiyo ya Samsung unaangaliwa kama utapunguza gharama za bei ya memori za ukubwa huo ambazo zipo sokoni kwa sasa ambazo zimekuwa zikuzwa kwa bei kubwa.

Memori kadi ya 512GB kwa sasa inapatikana kwa $300 ambazo ni sawa na shilingi ya kitanzania 685,000/-.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Mauzo ya simu yashuka robo ya kwanza ya mwaka 2019
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.