Tulio wengi tunafahamu matokeo ya kura ya Uingereza kujitoa/kubakia umoja wa Ulaya na kama utakumbuka asilima kubwa ya wananchi waliunga mkono mpango huo.
Hatua hiyo ya Uingereza kujitoa imetafsiriwa kama “Janga kwa taifa” pamoja na kwa wanasayansi ambao umoja huo uliwaleta karibu na wanasayansi wengine waliopo katika nchi wanachama wa umoja huo.
Ramani ya Umoja wa Ulaya huku Uingereza ikijiondoa kutoka kwenye muunganiko huo.
Hatua hiyo ya kujiondoa umoja wa Ulaya itaathiri uwekezaji katika tafiti za kisayansi ambazo huwa zinasaidia katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali, kilimo pamoja na viwandani. Pia hatua hiyo itaathiri uwezekano wa wanasayansi hao kuweza kusafiri bila VISA kutoka nchi mwanachama wa EU kwenda Uingereza au kutoka Uingereza kwenda nchi nyingine kutokana na kujitoa kwao.
Wanasayansi na watafiti zaidi ya 200 akiwemo mwanasayansi maarufu duniani marehemu Stephen Hawkings walipiga kura ya “Hapana” kupinga hatua ya Uingereza kujitoa katika umoja wa Ulaya na kusema hatua hiyo italeta madhara makubwa kwa Uingereza ambao wanategemea sana tafiti za Kisayansi.
Maneno ya Fizikia mmoja yakihirisha kuwa Uingereza inahitaji kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika tafiti za Kisayansi.
Umoja wa Ulaya ulikuwa unatoa msaada wa £1bn|$1.276bn kwa ajili ya kusaidia katika tafiti mbalimbali zenye manufaa kwa nchi hiyo na umoja huo kwa ujumla hapo awali. Hivyo Uingereza itabidi ijipange vyema ili kuweza kujitosheleza yenyewe bila kutegemea msaada kutoka Umoja wa Ulaya.
Nini maoni yako kuhusiana na Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya wewe kama mdau wa sayansi na teknolojia? Endelea kusoma habari mbalimbali kupitia TeknoKona.
Vyanzo: livescience, theguardian
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|