Tulishaandika kuhusu ujio wa simu ya kwanza inayotumia Android kutoka kampuni ya BlackBerry inayofahamika kwa jina BlackBerry Priv, sasa imefahamika itaanza kupatikana lini na itauzwa kwa bei gani.
BlackBerry Priv itaanza kupatikana kuanzia tarehe 6 mwezi wa kumi na moja na itauzika kwa bei ambayo wengi wameona ni ya juu sana, dola 699 za kimarekani – takribani Tsh Milioni 1.5. Wengi wanaona bei hiyo ni kubwa sana na angalau ingeanza kuuzika kwenye Tsh Milioni 1 kwani mafanikio ya kimauzo ya simu hii ni muhimu sana kwa kampuni ya BlackBerry ambayo imekuwa ikipata tabu kwenye biashara ya simu kwa miaka kadhaa kwa sasa.
Ukilinganisha iPhone 6S inaanzia kwenye dola 649, Samsung Galaxy Note 5 dola 696
Bosi mkuu wa kampuni hiyo alishasema ya kwamba kama hawatafanikiwa kimauzo na BlackBerry Priv basi wanaweza wakaachana kabisa na biashara ya utengenezaji simu. – Wanataka wauze angalau simu milioni 1 ili wasifikirie kuachana na biashara hii.
Kwa kiasi kingine bei hii inaonekana ni sawa pale inapolinganishwa na uwezo wa simu hiyo ambayo inakuja na teknolojia mbalimbali za kiusalama kutoka kampuni hiyo.
Sifa za BlackBerry Priv
- GB 3 za RAM
- Prosesa ya Snapdragon 808
- Diski uhifadhi – GB 32
- Kioo cha HD – inchi 5.43 1440p AMOLED
- Kamera ya nyuma ni MP 18 wakati ya selfi ni MP 2
- Uwezo wa kutumia kadi ya SD (Memori kadi)
- Android 5.1
Bila kusahau uwepo wa keyboard kwa wale wasiopenda sana kutumia kioo mguso (touch screen)
2 Comments