Kampuni ya Mozilla yazindua app yake mpya inayofanya kazi ya kiupekee katika ulinzi wa data za watumiaji, app inaitwa Firefox Lockbox. App hii itahifadhi taarifa za apps na akaunti (passwords za login).

Mozilla
App hii inapatikana katika programu endeshi za Android na iOS. Pia mozilla imesema kuwa app hii imeletwa kwa watumiaji wa kivinjari cha Firefox ambao wamefungua akaunti ya Firefox. Kwa kutumia Firefox Lockbox mtumiaji ataweza kuwa na hifadhi ya kumbukumbu za taarifa za akaunti kama vile barua pepe na nywila za kwenye tovuti mbalimbali au app anazotumia kwenye simu yake.
App hii inafanana na app nyingine zinazotumika kuhifadhi passwords (nywila) kama 1password au lastpass ingawa app hizi zina uwezo zaidi: wa kuongeza, kupunguza na kurekebisha nywila zilohifadhiwa.
App ya hii inawezesha mtu;
- kuangalia logins zilizohifadhiwa ndani ya kivinjari
- kufunga na kufungua apps zingine kwenye simu kwa kutumia fingerprint na FaceID
Je wewe ni mpenzi wa kivinjari cha Mozilla Firefox na umeipenda app yao mpya ya kuhifadhi logins(username na passwords) zako zote zilizofanyika ndani kivinjari au simu yako?
Download/Shusha – Google PlayStore | iOS