Na wewe ni moja ya watu wanaoteseka kucheza michezo mikali kwenye simu janja kwa kutumia ‘touch’ ya kioo cha simu yako? Fikiria kucheza game kama GTA, FIFA 16, PES16, CALL OF DUTY au michezo mingine mikali, kwa kutumia tu kioo cha simu yako. Wakati mwingine unaweza kushindwa kucheza vizuri au hata kuua kioo cha simu yako. Sasa, mbadala umepatikana.
Kwa mfululizo wa vifaa vikali vya simu na tabiti zako, sasa unaweza kucheza kwa kujiamini kwa kutumia padi za michezo, kama zile tunazochezea kwenye michezo ya Play Station, Xbox au ya Kompyuta.
Zifuatazo ni padi kali 6, ambazo ziko sokoni zinakazokufanya utamani kucheza siku nzima michezo mikali ya kwenye simu janja au tabiti yako.
- MOGA CONTROLLER
Hizi zinaendana na simu janja za Androids tu. Zina kishikio kinachoweza kuhimili simu janja zenye ukubwa wa hadi inchi 3.2. Lakini pia, kwa kuwa zinatumia kiunganishi cha Bluetooth, si lazima kuishikiza simu au tabiti yako ndio uweze kucheza. Zinatumia battery za AAA zenye uwezo wa kukaa na chaji hadi masaa 18.
- 60BEAT WIRED CONTROLLER
Hizi zina utofauti kidogo na Moga. Zenyewe zinatumia kiunganishi cha waya mwembamba wa millimeter 3.5 unaounganishwa katika tundu za earphones za iPad au iPhone yako. Usiwaze kuhusu sauti, kwani huja na kifaa maalum kinachokuwezesha kuchomeka earphones na padi hii kwa wakati mmoja. Hizi zinafanya kazi na vifaa vya IOS tu.
- PHONEJOY
Hizi zimekaa kwa staili flani inayokuwezesha mtumiaji kuweza kupachika kifaa chako, kama tabiti au simu janja yako zenye ukubwa tofauti katikati na ucheza. Unaweza pia kuifunga nakutumia kama padi za pc za kawaida. Zinaendana na Android, IOS, Windows au Mac kwa michezo ya kawaida pia.
- IMPULSE
Hizi ni padi ndogo zaidi kuwahi kutengenezwa kwa ajili ya simu janja au tabiti yako. Ni ndogo kiasi kwamba unaweza kuitumia kama kishika funguo zako. Hizi zimetengenewa kwa mfumo ambao unaweza kui’beep’ kwa kutumia simu janja yako, kama ikitokea umepoteza funguo zako ulizozishikiza kwenye padi hizi.
- STEEL SERIES FREE
Hizi zina vitufe 12 vya kubonyeza, vitufe vya analogi viweili, zinatumia kiunganishi cha Bluetooth kuunganiusha na simu janja au tabiti yako. Zinachajiwa na huweza kukaa na chaji hadi masaa 10. Uzuri wake ni kwamba, ni nyepesi sana, zina gramu 54 tu, na ni moja ya padi kali zaidi kwa ajili ya simu yako. Zinapiga mzigo wa Android, IOS, MAC au hata kompyuta yako ya Windows.
- ZEEMOTE
Ndio. Hizi ni padi za michezo kwa simu au tabiti yako pia. Hizi zimeundwa ili zitumike kucheza michezo kwa kutumia mkono mmoja pekee. Kutokana na upekee wake huo, inahitaji mda adi kuweza kuzoea kutumia padi hizi, japo ni bora zaidi kutumia kuliko padi za kwenye kioo cha simu yako ya android.
Je unapenda magemu kwenye simu janja yako kiasi cha kuitaji kutumia Gamepad? Tuambie maoni yako
Chanzo cha Makala haya ni mtandao wa PhoneArena.
No Comment! Be the first one.