Ndio! ni vizuri kuwa na simu kama Samsung na Apple lakini saa zingine inaboa kuona kitu kinachobadilika katika simu yako ni namba pale mwisho (katika jina) lakini mfumo mzima kiujumla ukiwa upo sawa.
Nakumbuka kuna watu hapo awali walihama kutoka katika kutumia Nokia kwenda katika Android Na walijetetea kwa kusema “Nimechoka na mfumo mzima wa nokia, Menu yake ni ile ile tuu”
Kuwa na machanguo mengi ni kitu kizuri. Unahama mda wowote unaontaka. Sasa kama simu tulizozoea kutumia ni zile za samsung yaani samsung Galaxy na iPhone vipi tukizichoka? — Au tutatumia huawei na tecno sio? — ni jambo zuri pia. Mimi napenda mabadiliko naamini ni vigumu sana kukaa na simu moja kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi miwili
TUZIJUE SIMU ZINGINE ZA MBADALA KWA SAMSUNG NA APPLE
Runcible

Nakumbuka Kijana Mokiwa wa TeknoKona aliandika kuhusu simu hiyo hapa. Ni simu flani hivi ya ajabu yenye umbo la mviringo. Kama unataka kujitofautisha na watu wengine wanavyotumia basi Runcible ni chaguo sahihi. Simu hii licha kuwa ya mviringo pia ina kava la ubao kwa nyuma. Ndio hutaweza kuangalia vitu kama video za 4K katika simu hii lakini tutegemee maboresho siku yeyote
Marshall London

Kama wewe ni Dj au ni mpenda muziki hii kwa ajili yako. Hii ni simu ya kwanza kutoka katika kampuni ya Marshall, simu hii ni maarufu kwa ‘Earphone’ zake na hata spika. Spika zake za nje ni kubwa sana na pia ina matundu mawili ya kuweka/kuchomeka ‘earphone’.
Fairphone 2

Kuna baadhi ya watu wanashindwa kuelewa kwanini simu nyingi zinatengenezwa china aua hata kama hazikutengenezwa china basi huwa sinaunganishwa china — au hata hivyo vyote vikishindikana hata betri basi lazima iwe imetoka china (haha!) — Sababu zipo nyingi moja katika ya hizo ni kwamba china kuna wafanyakazi/vibarua nafuu (cheap labor) na pia mazingira yanaruhusu. Simu hii ya Fairphoone imetolewa makusudi ili kuelezea mazingira ya kazini. Kampuni inafanya juu chini katika kuhakikisha kuwa wafanya kazi wanalipwa vziuri mishahara/vibarua vyao. Malighafi zake zinapatikana katika njia iliyosalama na pia imetengenezwa kwa kiasi kwamba hata ikiharibika ni rahisi kuirekebisha
Robin

Kama unapenda ku-save au ku ‘bakc up’ vitu aua taarifa zako katika mtandao kama vile Google Drive basi kuna hatihati kubwa ya kuipenda simu hii ya Robin. Simu hii imetengenezwa kwa kiwango cha hali ya juu na ina uwezo wa ku ‘back up’ kitu chochote yaani kuanzia Apps,muziki mpka picha. Kitu kingine ambacho ni cha aina yake katika simu hii ni kwamba inafuta kitu chochote ambacho hukitumii au hukiangalii mara kwa mara na inafanya hivyo mpaka uvihitaji vitu hivyo.
Turing Phone

Ni vigumu sana kuwaridhisha watumiaji wa simu janja siku hizi. Ni lazima uje na kitu cha kipekee katika soko la simu sio?. Simu hii ya Turing ina ‘Specification’ za aina yake na pia umbo lake limetengenezwa kwa kutumia ‘liquidmorphium’, mfumo mpya wa Alloy. Watengenezaji wake pia wanajifia kuwa wameweka hali nzuri ya kiusalama katika simu hii. Pia simu hii itajiunganisha na vifaa vingine inavyoviamini tuu na la mwisho ni kwamba simu hii ina chaja ya sumaku.
Mengi umeyoana kuhusu simu hizi kwa ufupi lakini swali ni je, unaishukia simu yako hivi sasa?. Simu hizi kwa wingi hazipatikani bongo ukitaka kuwa nayo ni mpaka uagize kutoka kwa watu weupe.
Tuambie katika ya hizi ipi imekuvutia wewe? Tandikie sehemu ya comment pia usisahao kutembelea mtandao wako pendwa kila siku. Kumbuka TeknoKona Tupo Nawe Katika Teknolojia
3 Comments