Canonical, shirika linalomiliki programu endeshaji maarufu ya Ubuntu iliyo katika familia ya Linux wamefanikiwa kuingiza sokoni simu ya kwanza inayotumia programu endeshaji (OS) ya Ubuntu. Na mafanikio yamekuwa makubwa sana kwani simu hiyo ilifanikiwa kuuza nakala zote walizokuwa nazo ndani ya muda mchache.
Programu endeshaji ya Ubuntu inategemea kuingia ushindani na za iOS na Android, je watafanikiwa? ni mapema sana kusema.
Simu hiyo kutoka kampuni ya Ulaya ya BQ inayofahamika kwa jina la BQ Aquaris E4.5 Ubuntu Edition iliuzika kwenye mtandao wa watengenezaji wa simu hiyo wiki iliyopita. Ubuntu wamejitahidi kwenye ubunifu wa kitofauti na mvuto, wanategemea kujifunza mengi kutoka mafanikio ya Android ambayo nayo imejengwa juu ya mfumo wa Linux.
Simu ya BQ Aquaris E4.5 Ubuntu Edition inapatikana kwenye soko la Ulaya kwa takribani dola za kimarekani 190, au Tsh laki tatu na nusu.
Sifa zake;
- Kioo cha inchi 4.5 (960×540)
- a quad-core 1.3GHz Cortex A7 CPU
- RAM GB 1
- Diski uhifadhi GB 8 (Unaweza tumia kadi ya SD hadi ukubwa wa GB 32
- Kamera ya nyuma ‘megapixel’ 8 na ya mbele megapixel 5
Mafanikio ya toleo hili yatasaidia kuonesha uhitaji (demand) na umaarufu wa programu endeshaji hii, yapo makampuni mengine ya simu yanayotegemewa kuleta simu zinazotumia Ubuntu kipindi cha mwaka huu na mwakani. Wengi wanataka Ubuntu ipate mafanikio katika soko linaloonekana kumilikiwa na Android na iOS kwa sasa, wengi wanasema ni muhimu kuwe na ushindani mkubwa wa kampuni tatu kuliko mbili.
Windows na BlackBerry OS hawajafanikiwa sana kuonesha ushindani wa uhakika na ujio wa Ubuntu unakaribishwa vizuri lakini ni ukweli usiopingika wana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha mafanikio ya programu endeshaji hii. Kampuni ya Canonical wamefanikiwa kuleta simu inayotumia ubuntu, sasa tunasubiri kuona ni jinsi gani watapigania mafanikio ya simu hizo.
Endelea kusoma TeknoKona!
No Comment! Be the first one.