fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
IPhone Nokia Samsung simu Tanzania Teknolojia

Simu 20 Zilizouzika Zaidi Duniani Hadi Sasa-Namba 10 hadi 1

Simu 20 Zilizouzika Zaidi Duniani Hadi Sasa-Namba 10 hadi 1

Spread the love

Wiki iliyopita tuliangalia namba 20 hadi 11 katika simu zinazoshikilia chati kimauzo duniani na leo tunaangalia namba kumi hadi moja, kwa kujikumbusha zilizoshika namba 20 hadi 11 unaweza BOFYA HAPA! Nokia iliingiza simu nne katika chati hiyo wakati Apple waliingiza iPhone tatu huku Motorola iliingiza simu mbili na Samsung iliingiza simu moja, je mambo yatabadilika katika 10 za juu? Endelea kusoma;

Nafasi ya 10 inashikiliwa na Nokia 3310 (3330) iliyotoka mwaka 2000 na simu hii iliuzika kwa zaidi ya nakala milioni 126. Hii bila ubishi wengi mtakuwa mnaikumbuka kwani hata nchini kwetu ilionekana karibia kwa kila mwenye simu enzi nzileeee 🙂

Nokia 3310

Nokia 3310

Namba 10: Nokia 3310

Ilitolewa Mwaka: 2000

Idadi ya Mauzo: Milioni 126

Nokia 1600 (1650/1661) iliyoingia sokoni mwaka 2006 inashikilia namba tisa kimauzo kwa kuuza takribani nakala milioni 130

Nokia 1600 ilitolewa kwa rangi tatu tofauti

Nokia 1600 ilitolewa kwa rangi tatu tofauti

Namba 9: Nokia 1600

SOMA PIA  BlackBerry yauza hakimiliki zake za thamani ya $600 milioni

Ilitolewa Mwaka: 2006

Idadi ya Mauzo: Milioni 130

Namba nane inashikiliwa na simu iliyouzika kuliko zote kutoka kwa Motorola, na hii ni Motorola RAZR V3 iliyotoka mwaka 2004.

Muonekano wa Motorola RAZR V3

Muonekano wa Motorola RAZR V3

Namba 8: Motorola RAZR V3

Ilitolewa Mwaka: 2004

Idadi ya Mauzo: Milioni 130

Simu nyingine kutoka Nokia inashikilia namba 7, na hii ni Nokia 2600 (2610/2626/2630) ya mwaka 2004..

Muonekano wa Nokia 2600. Simu hii ilikuwa nzuri kwa chaji na pia ilikuwa ni ya rangi.

Muonekano wa Nokia 2600. Simu hii ilikuwa nzuri kwa chaji na pia ilikuwa ni ya rangi.

Namba 7: Nokia 2600

Ilitolewa Mwaka: 2004

Idadi ya Mauzo: Milioni 135

Je unafikiri simu iliyouzika kuliko zote kutoka Samsung ni ya toleo la Galaxy? Hapana, ni Samsung E1100 iliyoingia sokoni mwaka 2009 na inashika nafasi ya 6 na siyo ya Android.

Kutokana na Kufanya vizuri kimauzo simu hii iliendelea kutengeneza kwa muda mrefu (2009-2012)

Kutokana na Kufanya vizuri kimauzo simu hii iliendelea kutengeneza kwa muda mrefu (2009-2012)

Namba 6: Samsung E1100

SOMA PIA  Fahamu idadi ya watu walioonyesha hisia zao kwenye WhatsApp

Ilitolewa Mwaka: 2009-2012

Idadi ya Mauzo: Milioni 150

Nafasi ya tano inaenda kwa Nokia 6600 iliyotoka mwaka 2003 na ilifanikiwa kuuza nakala milioni 150. Simu hii iliyokuwa inatumia programu ya uendeshaji ya Symbian ilikuwa moja ya simu ghari zaidi ilipotoka, ilikuwa inauzwa kwa zaidi ya milioni 1.2 za kitanzania.

Muonekano wa Nokia 6600

Muonekano wa Nokia 6600

Namba 5: Nokia 6600

Ilitolewa Mwaka: 2003

Idadi ya Mauzo: Milioni 150*

Nokia 5230 inashikilia nafasi ya nne kwa mauzo ya zaidi ya nakala milioni 150, simu hii ilitoka mwaka 2009

Muonekano wa Nokia 5230

Muonekano wa Nokia 5230

Namba 4: Nokia 5230

Ilitolewa Mwaka: 2009

Idadi ya Mauzo: Milioni 150*

Nokia 1200 iliyoingia sokoni mwaka 2007 inashikilia nafasi ya tatu kwa mauzo ya zaidi ya nakala 150. Je ulishawahi kutumia simu hii? Nakumbuka tatizo lake kubwa lilikuwa ni kuvimba kwa kipadi zake baada ya matumizi ya muda mrefu.

Muonekano wa Nokia 1200

Muonekano wa Nokia 1200

Namba 3: Nokia 1200

SOMA PIA  Vivo Kuja Na Simu Janja Ya Kujikunja Septemba 2022!

Ilitolewa Mwaka: 2007

Idadi ya Mauzo: Milioni 150*

Nafasi ya pili inakwenda kwa Nokia 3210 iliyoingia sokoni mwaka 1999 iliyofanikiwa kuuzika kwa zaidi ya nakala milioni 160.

 

Nokia 3210 inayoshikilia nafasi ya pili ni moja ya simu maarufu sana, na ilikuja na gemu la Snake enzi hizo

Nokia 3210 inayoshikilia nafasi ya pili ni moja ya simu maarufu sana, na ilikuja na gemu la Snake enzi hizo

Namba 2: Nokia 3210

Ilitolewa Mwaka: 1999

Idadi ya Mauzo: Milioni 160*

Nafasi ya kwanza inashikiliwa na simu mbili, zote kutoka Nokia. Hii ni kwa sababu taarifa zao za kimauzo zinautofauti utofauti kidogo na hivyo mara nyingi inakuwa ni bora kuziweka katika sehemu moja. Na hizi ni Nokia 1100 ya mwaka 2003 pamoja na Nokia 1110 ya mwaka 2005 na kila moja imeuza zaidi ya nakala milioni 250, hivyo kwa ujumla wake kuna zaidi ya nakala milioni 500.

Nokia 1110 ilitoka mwaka 2005

Nokia 1110 ilitoka mwaka 2005

Ingawa Nokia 1100 na 1110 zinaoneshwa Kushindania namba 1, sehemu nyingi kama Wikipedia wanaiweka Nokia 1100 namba moja kimauzo

Ingawa Nokia 1100 na 1110 zinaoneshwa Kushindania namba 1, sehemu nyingi kama Wikipedia wanaiweka Nokia 1100 namba moja kimauzo

 

Simu yangu ya kwanzu kutumia ipo katika orodha hii, wewe je? Na umegundua jambo moja katika orodha hii? – Nokia ndiye mwenye simu nyingi zaidi.

Kumbuka unaweza kujikumbusha nafasi ya 20 hadi ya kumi na moja kwa kubofya hapa – Hizi Ndizo Simu 20 Zilizouzika Zaidi Duniani Hadi Sasa!

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania