Baada ya kuona vita ya kufanya wanavyofanya Apple na Samsung imekuwa ngumu na isiyo na mafanikio kampuni ya BlackBerry imekuja na kitu kipya cha kipekee kupitia kifaa kinachoweza kuwa na sifa za fableti (‘phablet’) kinachokwenda kwa jina la BlackBerry Passport. Je BlackBerry passport ni sawa na Samsung Galaxy Note? HAPANA, BlackBerry Passport ipo ya kitofauti, na wachambuzi wengi wamediriki kusema ingekuwa Passport imetolewa na kampuni nyingine kama Samsung au kampuni ndogo basi ingepewa uzito zaidi wa kuongelewa kuliko inavyopata sasa.
Jina la Passport limetumiwa kutokana na simu hii kuchukua vipimo kama zile za shahada ya kusafiria maarufu kwa jina la Passport.
Je kuna nini kipya kwenye BlackBerry Passport?
Moja ya sifa kubwa ni uwepo wa kibodi (vibonyezo/keyboard). BlackBerry ndio wanashikilia sifa ya kuwa na kibodi zenye mvuto na uzuri katika utumiaji. Lakini pia kitu kipya katika kibodi hii ni kuwa inaweza kutumika kama ‘kipanya’ kwa kimombo ‘mouse’ kwa kupitisha kidole juu ya eneo la kibodi. Tazama hapa;
Utaweza kutumia Apps za Android
Bado BlackBerry hawajafanikiwa kuwavutia maprograma kutengeneza Apps kwa ajili ya BlackBerry OS hivyo BlackBerry wameongezea kitu kwenye OS yao kuwezesha programu za Android kutumika katika simu zao. BlackBerry Passport inakuja na soko la Apps la Amazon ambalo halina apps nyingi kama soko la Google Play ila lina apps za kutosha hii ikiwa ni pamoja na apps nyingi maarufu zinazotumiwa kila siku.
Imepewa sifa kubwa katika suala la utumiaji wa mtandao – intaneti, na inasemekana mitandao mingi inafunguka vizuri bila kuharibu mtazamo wake.
Mambo mengine mengi kama uwepo wa BBM hazijabadilika. BlackBerry Pocket inalenga watu wa kiofisini, unaweza ichukulia kuwa kama begi lako dogo. Wachambuzi wengi wamesoma ukubwa wake unaweza kuwa usumbufu kwa wengi pale linapokuja suala la utumiaji, kwani ni lazima utumie mikoni miwili, kwa ukubwa wake inajaa kiraisi kwenye kiganja kimoja – tazama picha.
KIBAYA zaidi kuhusu simu/fableti hii ni bei yake! BlackBerry Pocket inauzwa kwa takribani Tsh Milioni 1, na wengi wanasema kwa bei hii itakuwa vigumu kumfanya mnunuaji aache kununua simu za iPhone 6 Plus au Samsung Galaxy Note badala ya hii. Ata hivyo pia BlackBerry wanategemea kuwauzia watu wa kitofauti zaidi, wao wanaona simu hii ni kwa watu wa makazini, watu wanaotaka kufanya kazi na si vinginevyo.
Sifa zaidi ni kama hivi;
SIFA BLACKBERRY PASSPORT
Bei: Takribani milioni 1 (Dola 600 za Marekani)
Kioo: Inchi 4.5
Prosesa: Qualcomm Snapdragon 801 (2.26 Ghz)
RAM: 3GB
Diski Uhifadhi: GB 32 na sehemu ya kadi ya microSD (uwezo hadi kadi za GB 128)
OS: BlackBerry 10.3
Betri: 3,450mAh
Uzito: Gramu 194
JE UNADHANI HII SIMU ITAUZA? UKIWA NA MILIONI MOJA NA INABIDI UCHAGUE KATI YA SIMU HII NA TOLEO JIPYA LA SAMSUNG GALAXY NOTE AU IPHONE JE UTANUNUA IPI?
No Comment! Be the first one.