Watumiaji wa uhifadhi wa mtandaoni sasa wanazidi kurahisishiwa jambo hilo, tena haswa kwa wale wanatumia huduma ya Dropbox. Kwa sasa huduma hii inawawezesha kumtumia mtu picha, video au mafaili mengine kwa kutumia Facebook Messenger.
Ili kufanya hivi kupitia simu janja yako kuna App mbili za muhimu za kuwa nazo katika simu yako. App ya kwanza ni ile maarufu ya Facebook Messenger nay a pili ni Dropbox yenyewe. Zoezi hili litawezekana kwa watumiaji wa aina zote mbili za simu (Android na iOS).
“Tunataka kutumiana (kushea) mafaili kuwe rahisi kadri iwezekanavyo” – kampuni ya Dropbox ilisema
Huduma hii imeanza kupatikana Aprili 2 mwaka huu. Hii ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kwa mtandao wa Facebook kushirikiana na kampuni inayotoa huduma ya uhifadhi wa mtandaoni katika kushambaza huduma.
Ili kutuimia huduma hii mtumiaji itambidi aende kwenye sehemu ya ‘More’ akiwa kwenye Messenger. Baada ya hapo Dropbox itatokea kama moja ya machaguo. Kwa kuchagua kwenye Dropbox mtu atakuwa tayari kuweza kumtumia mtu mafaili yake aliyokuwa kaya hifadhi katika Dropbox.
Dropbox kwao wanasema hili ni jambo zuri sana kwani mtu utakuwa hauhifadhi tuu picha bali huduma hiyo inakupa uwezo wa kuituma kwa ndugu, jamaa na marafiki zako. Kwa mfano pata picha umeenda kujiburudisha na ukapiga picha tukio la aina yake. Tukio hilo unaweza ukalihifadhi na kulituma kwa watu haraka iwezekanavyo kwa msaada wa Facebook na Dropbox
One Comment
Comments are closed.