Hii sio rasmi sana lakini inasemekana kuwa kampuni ya Apple iko mbioni kuongeza idadi ya matangazo katika vifaa vyake vya iPhone na bidhaa zingine za Apple.
Kuna makala tulinadika kuhusiana na Apple kuweka matangazo ndani ya App Store kwenye kipengele cha Today, soma zaidi >>HAPA<<

Kwa sasa huko AppStore kama mwenye App anataka App yake itangazwe ndani ya soko hilo basi ana uwezo wa kulipa pesa kwa Apple na kisha wanamtangazia App yake.
Kumbe hali haijaishia hapo na sasa kinachofanyika ni kwamba watu wategemee matangazo zaidi katika baadhi ya huduma kama vile Maps, Podcasts na Books.
Kama ilivyo katika AppStore basi na hata katika Maps wafanya biashara wataweza lipia gharama ya matangazo ili huduma zao ziweze kuonekana kiurahisi.
Podcasts na Books pia vivyo hivyo, hii inatuonyesha kuwa teknolojia inavyozidi kukuwa katika makampuni haya hakuna vya bure bure tena sio?
Kumbuka huduma hizo tatu kutoka Apple mpaka sasa hazijawahi kujihushisha kabisa na matangazo hapo awali.
Kwa Apple hili ni jambo zuri kwani watajihakikishia sehemu zingine ambazo wanaweza wakawa wanajikusanyia mapato.

Ni wazi kuwa kwa sasa kampuni hiyo ya Apple ipo katika mkakati wa kuhakikisha kuwa inauza sehemu nyingi sana za matangazo ili wapate mapato makubwa
Hata katika huduma ya Apple Tv Plus bado kampuni inafikiria kunzisha kitu kama walichofnaya Neftlix, yaani kupunguza gharama ya kifurushi na kuruhusu matangazo.
Hii sio mara ya kwanza kuyaona makampuni makubwa sana katika maswala ya kiteknolojia kuanzisha njia mbadala katika kuhakikisha kuwa inaongeza idadi ya mapato katika kampuni husika.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Je unahisi ni sawa kwa kampuni kuweka matangazo ndani ya huduma hizo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.