fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Bastola Inayokunjika na kuchukua muonekano wa Simu-Janja, Ukaificha mfukoni!

Bastola Inayokunjika na kuchukua muonekano wa Simu-Janja, Ukaificha mfukoni!

Spread the love

Kampuni inayoitwa Ideal Conceal imetengeneza bidhaa yake ya kwanza, bastola inayoweza kukunjwa na kuonekana kama simu-janja ndani ya kasha yake (kava). ‘Pistol’ hiyo ni ya .368 na inajikamata kisawasawa iwapo imefunguliwa, kufanya isichezecheze.

Ukiifunga, sehemu ya kufyatua risasi inafichwa barabara na mkono wako, na hivyo kuonekana kama simu-janja. Pia, kipo hata kishikio cha bastola hiyo cha kiunoni chenye muonekano wa kishikio cha smu-janja.

Bastola Inayokunjika na kuchukua muonekano wa Simu-Janja

Bastola Inayokunjika na kuchukua muonekano wa Simu-Janja

Simu hiyo ya kijanja itapatikana nchini Marekani. Kwa sasa na kwa maana nzuri zipo sheria zilizopitishwa na maeneo husika (majimbo) kuzuia au kudhibiti silaha zenye mfumo wa kufichika.

SOMA PIA  Jinsi ya kuwa na akaunti ya kibiashara ya Youtube #Maujanja

Bastola Inayokunjika na kuchukua muonekano wa Simu-Janja

Tovuti ya yahoo.com inakariri meneo ya kwenye tovuti ya kampuni ya Conceal yanayosema kwamba, “Wazo la Ideal Conceal linaendana na ongezeko la mahitaji ya bastola ambazo watu wanaweza kubeba kirahisi kila siku. Kuanzia wakina-mama wa nyumbani na hata watu wa kazi maalumu za kila aina , hii bastola inakupa chaguo la kutokuwa mhanga.”

Kwa muda huu, pistol hizi bado ziko matengenezoni na hazijatolewa kwa ajili ya mauzo, hatahivyo, kampuni ya Ideal Conceal inategemea kuanza kuziuza katikati ya mwaka 2016. Kupitia mahojiano na CNNMoney, imejulikana kwamba mmiliki wa kampuni, Kirk Kjellberg amepokea barua pepe 2,500 kutoka kwa watu wanaotaka kununua silaha hiyo.

SOMA PIA  Mwamvuli Janja usiobebwa kwa mkono

Je, unaoanaje ubunifu huu. Unakubaliana na kuwepo kwa silaha kama hizi nchini kwako? Una habari nyingine za ubunifu katika teknolojia kama hii?

ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comment

Comments

  1. […] post Bastola Inayokunjika na kuchukua muonekano wa Simu-Janja, Ukaificha mfukoni! appeared first on […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania