Kumbuka India ndio soko la tatu kwa ukubwa duniani katika biashara ya simu janja. Katika hii vita ya nani anashakili kwa kiasi kikubwa soko hilo Apple ametupwa mbali na mpinzani wake wa siku zote (Android).
Ni wazi kwamba simu nyingi zinazotumia programu endeshaji ya Android huwa zinapatikana kwa bei ya chini kidogo ukilinganisha na zile za iOs. Hii inaweza ikawa ni sababu moja wapo ya kushuka kwa soko hilo kwa upande wa Apple kwani India bado kuna watu masikini sana.
Robo ya pili ya mwaka 2016 Apple ilipeleka simu 800,000 nchini India lakini ukiangalia namba hii ni ndogo sana kwani msimu huo huo mwaka jana Apple waliingiza simu milioni 1.2
Kushuka huku kwa mauzo inamaanisha wapinzani wao wanawapita. Na hapa haimaanishi ni Samsung peke yao (kumbuka simu nyingi zinatumia Android).
Mtandao wa The Verge ulitoa taarifa kuwa India kwa mwaka huu (2016) inategemea kununua simu milioni 139, lakini wingi wa simu hizi zitakuwa ni zile za Android tena ambazo zina gharama ya chini kabisa (dola 150 za kimarekani).
Bado taarifa hizo hizo zinasema kuwa kampuni ya Google chini ya programu endeshaji yake ya Android inatumika kwa asilimia 97 katika soko.
Hiyo ni asilimia nyingi sana kwa mtu ambae unashindana nae sio? Kumfikia na kumpita tena inakuwa ni vigumu eeeh? Lakini katika swala zima la Teknolojia hilo sio jambo la kufikiria sana. Ni ubunifu tuu unaohitajika na Apple wanaweza wakafikia namba hiyo na kuipita
Kabla hujabisha! Labda nkuulize hivi kuna mtu alikuwa anajua kama Nokia inaweza ikaja kuuza kitengo chake cha simu na simu janja? Kumbe kila kitu kinawezekana katika teknolojia. Basi tukae tukisubiria kuona vita hii itafikia wapi