Neil Armstrong alikuwa ndiye mwanadamu wa kwanza kukanyaga ardhi ya Mwezi, mengi yamekwisha fanyika baada ya safari hiyo ya kihistoria na bado mengi yanafanyika hasa katika jitihada za kufanya makazi. Profesa Stephen Hawking amezindua misheni ya kwenda katika nyota iliyo karibu kabisa na mfumo wa sayari.
Nyota zipo umbali mrefu saana kutoka katika dunia, na hii ndiyo imekuwa kikwazo kikubwa kwa wanasayansi kuzifikia na kuzichunguaza zaidi. Nyota iliyo karibu zaidi inaitwa Alpha Centauri ambayo ipo katika umbali wa maili trilioni 25 kutoka duniani.
Pamoja na umbali huo wapo wanasayansi ambao wanalenga kuifikia nyota hii ili kuweza kuanza kuifanyia uchunguzi mbalimbali, Profesa Stephen Hawking amezindua misheni ya kwenda katika nyota kwa kupeleka chombo ambacho kitaenda kwa kasi kubwa zaidi leo.
Tayari kipo chombo kilicho pewa jina la Voyager ambacho kwa mwendo kinaoenda sasa kitatumia miaka 30,000 kufika katika nyota hiyo ambayo ndiyo ipo karibu zaidi.
Misheni iliyozinduliwa siku ya jumanne inahusisha chombo kilichopewa jina la “nanocraft” kinategemewa kufanya misheni ya kwenda katika nyota kwa kutumia muda wa miaka 20 kufika, pengine unaona huu ni muda mrefu saana ila katika teknolojia wakati mwingine unahitaji uvumilivu wa hali ya juu na huu ni mfano tu.
Mpango huo unapewa sapoti pia na muanzilishi wa mtandao wa Facebook, bwana Mark Zuckerberg
Misheni hii itagharimu zaidi ya Dola milioni 100 ambazo zimetolewa na bilionea wa kirusi Yuri Milner na imepewa jina la Starshot. Na katika halfa hiyo bilionea huyo alisema kwamba swali la msingi ni kujiuliza kama kweli tunaweza kuzifikia nyota na kama kweli tunaweza kuzifikia nyota katika kipindi cha maisha yetu?
Nanocraft itakuwa inaendeshwa kwa nguvu za jua ambazo zinapatikana kutoka katika mwale wa laser unaorushwa kutoka duniani ili kufanikisha misheni hii na itakuwa ninakwenda kwa mwendo kasi wa kilomita milioni 100 kwa saa.
Katika tafrija hiyo Profesa Stephen Hawking alizungumzia juu ya uwezo wa binadamu kutokubali kuzuiliwa na changamoto tunazokutana nazo.
Upo hapo? Je unaona ni sahihi kutumia mabilioni ya pesa katika kutafuta maisha mengine nje ya dunia? au pesa hizo zitumike kuboresha maisha ya hapa hapa?
Makala hii imeandikwa kwa msaada wa mtandao na pia Jarida la The Telegraph.
One Comment
Comments are closed.