fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple iOS Mtandao wa Kijamii

Pengine Tusahau Kabisa iMessage Kwenye Vifaa Vya Android!

Pengine Tusahau Kabisa iMessage  Kwenye Vifaa Vya Android!

iMessage ni huduma ya kutuma na kupokea ujmbe (inajumuisha maandishi, video na picha) katika vifaa vya iOS tu. Huduma hii imekua maarufu sana na inawafanya hata watumiaji wengi wa vifaa vya iOS kutohama na kwenda katika vifaa vingine kama vile vya Android.

Hapo awali kulikua na fununu nyingi sana ziliingia kwamba pengine labda Apple wangepeleka huduma yao hiyo kayika programu endeshaji ya Android. Hiyo ni sawa ingewaongezea watumiaji wengi sana wa huduma hiyo.

iMessage

Tofauti Ya Kimuonekano Kati Ya iMessage (bluu) Na Meseji za Kawaida (Kijani)

Lakini Apple wanasema kwamba wakiamua hivyo hilo litawaumiza sana kuliko kuwasaidia. Hii ni kwa mantiki kwamba sawa wataongeza watumiaji (Android) lakini watu wengine wanaweza wakahama kutoka kutumia iPhone na kuhamia simu zingine kama vile Samsung.

Kama huduma itapaikana kila sehemu basi soko la simu za iPhone litashuka wakati huo huo iMessage itakuza watumiaji wake na jambo hili litawaumiza sana Apple kuliko kuwasaidia.

iMessage

Muonekano Wa iMessage

Apple walikata kuanzisha iMessage kwa ajili ya Android tangu mwaka 2013. kumbuka huduma kama iMessage na Facetime ndio zinawafanya watumiaji wa iPhone, iPad, na Mac wazidi kubaki na kutumia vifaa hivi (labda wana sababu zingine) pengine wangeshalihama kama zingepatikana kwingine.

SOMA PIA  Facebook kuzuia akaunti Feki

Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Niandikie Hapo Chini Katika Sanduku La Maoni, Pia Tembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Vyanzo: HTech, MacRumors

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania