fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Facebook instagram Teknolojia whatsapp

Tatizo la muda kwa Facebook, WhatsApp na Instagram

Tatizo la muda kwa Facebook, WhatsApp na Instagram

Unafahamu kuwa Facebook, WhatsApp na Intagram zilikumbwa na tatizo la muda lililosababisha mawasiliano kuwa magumu? Wengi walipata changamoto duniani kote.

Katika mawasiliano ya wengi kwa miaka mingi tuu sasa yanafanyika kwa wingi zaidi kupitia WhatsApp halikadfhalika Instagram na Facebook ambazo zimekuwa na mchango wa kipekee katika kufanya watu wawasiliane kwa wepwsi kabisa. Sasa hakika wale ambao kwa namna moja au nyingine tulikuwa tukiperuzi kwenye WhatsApp, Facebook na Instagram mishale ya saa 7 usiku siku ya Alhamisi basi tulipata changamoto kwani mitandao hiyo ya kijamii ilikuwa na shida.

Ripoti zinaonyesha tovuti ya Facebook ilikuwa na matatizo zaidi ya 112,000 yaliyoripotiwa, 101,000 ya watumiaji wa Instagram na 516 ya watu kwenye WhatsApp walieleza changamoto walizokumbana nazo nyakati za saa 7 usiku wa Alhamisi.

Tatizo la muda

Ujumbeulikuwa umehusisha tatizo la muda ulionekana siku ya Alhamisi nyakati za saa 7 usiku kwa wale waliokuwa wakitaka kuingia kwenye akaunti zao za Facebook.

Hii imekuwa ni mara ya pili kwa tatizo hili kujitokeza katika kipindi cha karibu mwezi mmoja; katikati ya mwezi Machi changamoto hiyo ilijitokeza kwenye Facebook, WhatsApp na Instagram na kudumu kwa karibu saa nzima. Facebook walikuwa kimya tuu lakini inaaminika wahusika walikuwa kwenye zoezi za kuhifadhi taarifa za watumiaji wake ndio maana zoezi hilo likaleta malalamiko kutoka sehemu nyingi duniani.

Tuambie ewe msomaji wetu je, na wewe ulikuwa mhanga wa kutoweza kutumia Facebook, WhatsApp na Instagram siku ya Alhamisi mishale ya saa 7 usiku?

Vyanzo: Gadgets 360, Forbes

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania