Kama kuna simu ambayo imetokea kununuliwa kwa wingi sehemu nyingi duniani kwa simu janja za familia ya iPhone, iPhone 6 na 6+ inaongoza kuliko hata iPhone 7 na wengi ukiwauliza wanasema hakuna mabadiliko makubwa kati ya iPhone 6 na 7.
Apple imekuwa ni moja ya kampuni ambayo imekuwaikifanya vifaa vyake kutumika kiurahisi ingawa ili kuweza kujua namna gani unaweza kutumia kiurahisi ni lazima uwe mjanja mjanja au ufuatiliaji wa masuala ya teknolojia kama tulivyo TeknoKona.
Njia fupi 10 ya kufanikisha mambo mbalimbali kwenye iPhone 6/6 Plus.
>Kuwasha/kuzima mfumo wa kusahihisha neno kwenye sms
Ni jambo linalowakera watu wengi pale unapoandika ujumbe mfupi wa mameno na mara tu unapobonyeza kitufe cha kusogea mbele unashangaa neno husika linabadilika na kusahihisha neno husika kwa jinsi ilivyokisia kuwa ulikuwa unataka kuandika neno fulani.
Kwa kubonyeza kwa sekunde kadhaa kwenye sehemu ya kuandika sms itatokea menyu ndogo na sehemu Predictive utasogeza mbele kuweza kuwasha au kuzima.
>Kupiga picha zaidi ya mara moja kwa wakati mmoja
Kwa yeyote yule anayetumia iPhone 6/6+ anaweza akafanikisha jambo hili, kwa wale mnaopenda kupiga picha sana (photogenic) mtakuwa mmefurahi au sio? 😀 😀 . Cha kufanya ni kushikilia kitufe kilichoandikwa “Shutter” au kitufe cha chini cha sauti moja kwa moja mpaka pale utakapoamua kusitisha zoezi zima.
>Kuwa na nakala ya picha/picha jongefu zinazofanana
FIkiria pale unapotaka kuhariri picha/video fulani ili kuiongezea nakshi nakshi lakini kabla ya kufikiria kuongezea vitu fulani fulani kwenye picha/video husika ni muhimu ukawa na nakala halisi ya picha/video kwa kumbukumbu na matumizi mengine hapo baadae. Ukishachagua picha/video kutoka kwenye ‘Photos’ bofya palipoandikwa Shares (upande wa kushoto chini) kisha chagua Duplicate.
>Kuweka aina ya mtetemo (vibration) unaotaka mwenyewe
Vibration katika simu zetu zimekuwa msaada mkubwa kwetu hasa pale unapokuwa mahali ambapo hapahitaji kelele za hapa na pale hivyo tumekuwa tukizipangilia simu zetu katika mfumo wa mtetemo. Kwenye iPhone 6/6+ unaweza ukatengeneza mtetemo wa aina yake uliotengeneza mwenyewe. Ingia Settings>>Ringtone kisha chagua mlio unataka kuweka. Bofya “Create New Vibration” ili kuweza kutengeneza mtetemo unaotaka.
>Kuweka/kupangilia simu yako nyakati za usiku
Kuweka simu yako katika mfmo wa ‘Night mode’ kutasaidia kupunguza kiasi cha chaji ambacho kingeweza kutumika iwapo hujaweka katika ‘mfumo wa usiku’. Kwa kupangilia mfumo wa usiku simu yako itaweza kuchagua rangi nzuri na muonekano wa kuvutia kwa ujumla jambo ambalo litafanya simu yako iwe na muonekano wa kipekee.
Nenda kwenye Settings>>Display&Brightness>>Night shift>>Schedule. Kisha weka mpangilio wa usiku unapenda uanzie saa ngapi.
>Kuweka nywila kwenye taarifa fupi fupi (Notes)
Kuanzia toleo la iOS 9.3 unaweza kuweka nywila (password) kwenye yale mambo yako unayoandika kwa ajili ya kukumbuka hapo baadae. Hatua za kufuata ni kuingia Settings>>Notes>>Password. Weka password unayotaka ili kuweza kulinda taarifa zako kwenye kipengele cha Notes.
>Kurudi juu (mwanzo) kwa kutumia mkono mmoja
Kitu kingine cha kufurahisha na ujanja unaweza kufanya kwenye iPhone 6/6+ ni iwapo unataka kurudi mwanzo kabisa wa ukurasa fulani, shikilia kwa muda kidogo (kwa dole gumba) halafu fanya kama unavuta chini kidogo kisha achia, hapo utaona umerudi juu kabisa (mwamzo wa ukurasa husika).
>Jinsi ya kutoka kwenye jume za makundi kwenye iMessage
Moja ya vitu ambavyo vimerahisisha mawasiliano hasa kama utataka kuwasiliana na wengi kwa wakati mmoja ni jumbe za kwenye makundi na kwa wanaotumia iPhone wanafahamu kuhusu iMessage. Ukitaka kutoka kwenye mfumo wa makundi kwenye iMessage bofya Details (upande wa kulia juu) kisha chagua “Leave this conversation”.
>Kuchukua picha ya mnato (video) kwa mwendo wa polepole
Kipengele hiki hakikuwepo kwenye matoleo ya nyuma (kabla ya iPhone 6) ila kwenye familia ya iPhone 6 unaweza kuchukua video kwa mwendo wa polepole (slow motion). Kufanikisha kuchukua picha jongefu katika mfumo wa polepole ingia kwenye uwanja wa kamera na kisha hamisha simu yako kwenye upande wa video kisha bofya palipoandikwa SLO-MO kwenye kioo.
>Kuzuia watu wengine kukusanya taaarifa unapokuwa mtandaoni
Wanaotumia bidhaa za Apple Safari ndio kivinjari ambacho kinakuja kwenye bidhaa za Apple. Ukusanyaji wa taarifa za tovuti gani umetembelea/zipi unapenda kutembelea mara kwa mara limekuwa ni tatizo ila Apple wana suluhisho la kukufanya taarifa zako kuchukuliwa na wengine.
DuckDuckGo ni kivinjari kinachosaidia kuficha watu wengine (third parties) taarifa zako mbalimbali kutoka kwenye simu yako. Ingia Settings>>Safari na kisha badilisha tovuti ya kwanza kufunguka unapofungua kivinjari cha Safari badala wa Google chagua DuckDuckGo.
Ni matumaini yangu umepata ujanja wa kutumia kwenye iPhone 6/6+, pia kumbuka kuna mengi hapa yanaweza pia kutumika kwenye matoleo mengine ya iPhone.
Je, una maoni? Niandikie hapo chini na unaweza kutufuatilia kupitia Facebook, Twitter na hata Instagram.
Chanzo: Digital Trends
3 Comments
Comments are closed.