fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

simu Teknolojia

Yafahamu ya muhimu kuhusu Samsung Galaxy F12 na F02s

Yafahamu ya muhimu kuhusu Samsung Galaxy F12 na F02s

Moja ya simu ambazo zipo kwenye vinywa vya watu (zinazungumzwa kwa wingi) ni Samsung Galaxy F12 na F02s ambazo zimetoka kwa mkupuo tayari kwa kupata wateja lukuki duniani kote.

Moja ya vitu ambavyo vinafanya biashara nyingi kukua/kutengeeneza faida kubwa ni jinsi ambavyo wanajua kuendana na kile ambacho watu wanahitaji kwenye soko ambalo kila leo linapokea ushindani wa bidhaa kutoka kampuni mbalimbali duniani. Samsung wameamua Galaxy F12 na F02s ziwe na sifa hizi:

SOMA PIA  Bongoline: Je Watanzania tumevutiwa?

Sifa za Samsung Galaxy F12

Kioo :
 • Ukubwa: inchi 6.5
 • Ubora: 720×1600 px, ung’avu wa hali ya juu sana
Memori :
 • Diski uhifadhi: 64GB/128GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada mpaka TB 1
 • RAM: 4GB
Kamera :
 • Kamera Kuu: Megapixel 48, 5, 2 na 2
 • Kamera ya Mbele: Megapixel 8
Betri/Chaji :
 • Li-Ion 6000 mAh
 • USB-C+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 15W
Kipuri mama :
 • Exynos 850 SoC

Programu Endeshi

 • One UI 3.1, Android 11
Rangi/Bei :
 • Nyeusi, Bluu na Kijani
 • GB 4/64-$150 (zaidi ya Tsh. 345,000) na GB 4/128-$163 (zaidi ya Tsh. 374,900) bei ya ughaibuni
  Galaxy F12 na F02s

  Hiyo ndio Samsung Galaxy F12+ipo sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, inatumia kadi mbili za simu, WiFi, Bluetooth, 4G LTE.

   

Sifa za Samsung Galaxy F02s

Kioo :
 • Ukubwa: inchi 6.5
 • Ubora: 720×1600 px, ung’avu wa hali ya juu sana
Memori :
 • Diski uhifadhi: 32GB/64GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada mpaka TB 1
 • RAM: Gb 3/4GB
Kamera :
 • Kamera Kuu: MP 13, 2 na 2
 • Kamera ya Mbele: MP 5
Betri/Chaji :
 • Li-Ion 5000 mAh
 • USB-C+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 15W
Kipuri mama :
 •  Snapdragon 450 SoC

Programu Endeshi

 • One UI, Android 10
Rangi/Bei :
 • Nyeusi, na Bluu 
 • GB 3/32-$123 (zaidi ya Tsh. 282,900) na GB 4/64-$136 (zaidi ya Tsh. 312,800) bei ya ughaibuni
  Galaxy F12 na F02s

  Samsung Galaxy F02s+ipo sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, inatumia kadi mbili za simu, WiFi, Bluetooth, 4G LTE.

   

Hizo ndio rununu mbili kutoka kwenye familia ya “F” ambapo Galaxy F12 inafanana na Galaxy M12 huku F02s ikilandana na M02s.

TeknoKona tumeshakuhabarisha, vingine tunakuachia wewe msomaji wetu. Usisahau kusambaza kwa wengine makala zetu kwa wengine.

Vyanzo: Gadgets 360, GSMArena

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

 1. Bahebe Kidesheni - April 10, 2021 at 16:58 - Reply

  Shukrani kwa kuelimisha umma,vp kuhusu samsung galaxy M62?

  • Samsung Galaxy m62 taayri tulishaichambua. Angalia kwenye kiunganishi hiki kuweza kufahamu undani wake>>>https://teknolojia.co.tz/sifa-za-ndani-kuhusu-samsung-galaxy-m62/. Ahsante.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania