fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kompyuta Maujanja Windows

QuickLook – Wezesha ‘Preview’ kwenye Windows kwa kutumia Spacebar. #Maujanja

QuickLook – Wezesha ‘Preview’ kwenye Windows kwa kutumia Spacebar. #Maujanja

QuickLook ni kaprogramu kadogo kanakoleta uwezo mmoja mzuri ambao kwenye programu endeshaji ya MacOS kuja kwenye Windows.

Kupitia QuickLook hautakuwa na ulazima wa kufungua faili la picha au video wakati lengo lako lilikuwa kutafuta faili ambalo ni sahihi.

quicklook

Programu hii ni ya ukubwa mdogo na baada ya kuipakua kwenye kompyuta yako hauitaji kuifungua tena. Inakuwa inafanya kazi bila kuonekana, mfano kwenye file ya picha unataka kuingalia kama ni ndio inayoitafuta au la, itakubidi tu ubonyeze Space Bar ili kuweza kuifungua, na ukibonyeza Space Bar mara ya pili itafungwa. Unaweza kufanya hivyo kwa mafaili mengi mbalimbali kama vile ya muziki, video, documents n.k.

Programu hii inapatikana bure kupitia soko la apps la Windows. Pakua bure – QuickLook.

Fahamu maujanja mengine mbalimbali kwenye Windows – Teknokona / Maujanja

Je umejifunza kitu kipya leo? Tuambie ni nini kingine ungependa kufahamu zaidi? Tupo hapa pamoja na wewe.

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania