fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple IPhone

Jinsi Ya Kuipata iPhone Yako Hata Kama Imezimwa! #FindMyiPhone

Jinsi Ya Kuipata iPhone Yako Hata Kama Imezimwa! #FindMyiPhone

Spread the love

Hivi unajua kwa matoleo mapya katika simu kutoka kampuni ya Apple maarufu kama iPhone unaweza kuipata simu — ikiwa imezimwa — yako hata kama imeibiwa au umeishahua mahali.

Hii inaweza kupatika kwa toleo jipya la program endeshaji ya iOS 15.  hapa kinchofanyika ni kwamba utaweza kujua simu yako iliyo hata kama betri itakua imezima.

Kingine ni kwamba hili litawezekana katika baadhi ya matoleo ya simu za iPhone

  • iPhone 11
  • iPhone 11 Pro / iPhone 11 Pro Max
  • iPhone 12 / iPhone 12 Mini
  • iPhone 12 Pro / iPhone 12 Pro Max
  • iPhone 13 / iPhone 13 Mini
  • iPhone 13 Pro / iPhone 13 Pro Max
  • Na matoleo mengine yajayo

Kingine ni kwamba kama unatumia matoleo hayo na ios 15 kama progamu endeshaji basi utakapo kuwa unazima simu yako utapata ujumbe unaonema “iPhone Findable After Power Off’, hii ikiwa inamaanisha kuwa simu itaweza kupatikana hata kama ikiwa imezimwa.

Find My iPhone

Find My iPhone

Ili kuwezesha hili pia ni lazima uwe umewasha app ya ‘Find My iPhone’ na pia uende katika settings za ‘Apple ID’ na uweke ‘Share My Location’

Find My iPhone..

Find My iPhone..

Kama umefanya yote hayo basi pindi ambapo simu yako itakua imezimika/imezimwa na hujui iko wapi unaweza ukaingia katika mtandao wa http://icloud.com/find kupitia kompyuta.

Find My iPhone Katika Kompyuta

Find My iPhone Katika Kompyuta

Kinachofanyika hapa ni kwamba, kabla iPhone yako haijazima — simu kama simu — itaweza kutuma taarifa za eneo ambalo imezima katika hifadhi ya Apple.

SOMA PIA  Apple kuzuiwa kuuza iPhone 6 na 6 Plus Nchini China Kisa Wizi wa Ubunifu

Ambapo ukiamua kuingia kwenda kuifuatilia katika Find My iPhone Katika Kompyuta utapata eneo la mwisho ambapo simu hizo imezimikia.

Ningependa kusika kutoka kwako niandike hapo chini katika eneo la comment hii umeipokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Teknokona, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

SOMA PIA  Apple: Hivi Karibuni Utaweza Kuchaji iPhone na MacBooks Mara 1 Kwa Wiki

  Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania