OperaMini 7 |
Mwanzo wa mwezi huu ulikaribishwa na toleo jipya la OperaMini, browser ya intanet kupitia simu. Hakuna ubishi ya kwamba watu wengi zaidi, hasa katika nchi zetu zinazoendelea tunaingia kwa intaneti kutumia simu zetu kupita vifaa vingine. Na hapo ndo inapokuja OperaMini, lakini si hivyo tuu kwa wale watumiaji wa laptops na kompyuta za mezani(desktops) Opera wametoa toleo jipya la Opera 12.
Na kiukweli Opera kwa kompyuta/laptop sijawahi kuwa mpenzi wa kuitumia sana, na si mimi tuu ila ata kwa watu wengi zaidi duniani kutokana na data za kuilinganisha na Firefox, Chrome na hata IE. Lakini kwa toleo hili jipya nadhani wamenipata, since ku’install kwa laptop yangu sijatumia browser nyingine yeyote. Kwa kweli toleo hili ni la kitofauti na la kuvutia.
Opera 12 |
OperaMini 7:
-
Imekuja kitofauti, mabadiliko ya muonekano tokea OperaMini6
- Ipo ki’jamii zaidi, ina eneo la kukuunganisha na akaunti zako za kijamii kwenye sura ya mwanzao kabisa..Google+, Facebook, Gmail na mengineyo.
- Kama kawaida, unaweza pata habari/ma’news kwa uraii sana, za aina zote na eneo ‘spesheli’ la habari za michezo.
- Pia kuna kitu kinaitwa ‘Speed Dial’, hizi ni ‘shortcut’ za mitandao unayotembelea zaidi kama hapa juu kwenye Opera 12, sasa hii imeingizwa kwenye OperaMini kwa uzuri sana, utaona zaidi ya mitandao kumi unayotembelea zaidi kwa haraka.
- Na zaidi ya yote kuna ‘feature’ moja inayonifanya nimeamua kuendelea kutumia OperaMini na Opera ya kompyuta, nayo ni kupitia kutengeza akaunti na kuziunganisha opera zako kiasi ya kwamba unaweza tumia OperaMini afu ukaja kwa kompyuta na kuona ‘bookmarks’, historia, na vinginevyo kama kwenye OperaMini na vivyo hivyo kama ukifanya mabadiliko kwa Opera ya kompyuta, yataonekana kwa OperaMini pia.
Baada Ya Kubadilisha Theme |
- Kama umeshawahi kutumia Opera kabla utagundua mabadiliko mengi mazuri kwa Opera hii, kwanza imekuwa ndiyo browser ya kwanza ambayo themes zake zinaivalisha yote, na sio pande za juu na chini tuu kama zilivyo zingine kama FIrefox na Chrome.
- Na tayari ‘themes’ zake zipo kwa mamia, kazi kwako.
- Pia sasa unaweza ku’search kwa kutumia ‘address bar’
Kwa Opera 12 ya Linux, Windows au Mac unaweza ipata kwa kutembelea
pia kwa wale wenye simu za kisasa wanaweza tembelea
ili ujipatieOperaMini 7!
No Comment! Be the first one.