Umeipata hii? Saa nyingine hauwezi kukataa ya kuwa tukija katika masuala ya sheria za mawasiliano nchi yetu ipo poa sana, kwani kama ungekuwa Ethiopia ujue ukikamatwa unatumia huduma za intaneti za mawasiliano kama Skype na Google Talk (pamoja na huduma ya Google Hangout) unaweza shtakiwa kwenda jela miaka 15.
Sheria hiyo ilipitishwa kwenye mwezi wa tano kwa ‘gia’ ya usalama wa taifa. Lakini pia wachunguzi wanadai ni pamoja na kulinda soko la kampuni pekee ya simu imilikiwayo na serikali iitwayo Ethio Telecom, na sababu nyingine ni kuzidi kuwadhibiti wapinzani na wanaharakati wengine.
Kwa hiyo tuseme asante kwa taifa letu hili, kwani uwe google +, twitter, facebook, mig33 au Jamii Forums, hakuna akubanaye au anayekubania kuzipata huduma hizi!
Au sioooooo!!!!!! Kwani nadhani hata mimi hii miaka 15 ingenihusu, hahahahahahaha!!!!!!!
Nawatakia wiki njema!!
No Comment! Be the first one.