Chapa rasmi ya Windows 8 |
Weka viganja vyako tayari kwani Microsoft inajiandaa kukuletea Operating system nyingine katika mwendelezo wake wa familia za Windows. Operating system hii mpya itaitwa Windows 8. Microsoft inautangaza huu ujio mpya wa operating system ya Windows kama wazo jipya kabisa na la kipekee ambalo halijawahi kutokea katika ulimwengu mpana wa teknolojia ya kompyuta.
Pamoja na hayo, Microsoft wanategemea kwamba Windows 8 italeta ushindani zaidi katika soko linaloendelea kukua la vifaa-kompyuta vya kiganjani, vifaaa ambavyo vina uwezo unaokaribia kama sio sawia na kompyuta kubwa, vinavyojulikana kama mobile devices (tamka: mobaili divaisezi). Soko hilo kwa sasa linaongozwa na kampuni ya Apple (na bidhaa zake za iphone na ipad), kampuni ya Google (Kupitia Operating system yake Android amabayo inatumika kwenye simu nyingi, ikiwemo aina tofauti za Samsung, HTC na kampuni nyingine nyingi) na kampuni ya RIM (watengenezaji wa Blackberry).
Windows 8 kwenye kifaa-kompyuta cha kiganjani |
Tayari Microsoft imetoa toleo la majaribio la Windows 8, bure kabisa kwa ajili ya kukusanya maoni kutoka kwa wadau. Toleo hili lilitolewa februari 29 mwaka huu huku wakitegemea kutangaza windows8 rasmi October mwaka huu, itakayotolewa kwa matoleo matatu tofati kwa matumizi yanayotofautiana. Windows 8 itakuwa na muonekano mpya kabisa na utakohitaji mtumiaji auzoee kidogo kabla ya kuuelewa kabisa. Microsoft wameelezea kuwa wametumia mfumo mpya wa mitindo kutengeneza operating system hiyo uitwao Metro ambao wametumia kutengeneza kiolesura kitakachotumia jina hilo hilo, kiolesura cha Metro. Kiolesura hiko kitaonekana kuwa na vigae vya pembenne kwenye skrini ambavyo kitawakilisha programu ambazo zimo kweye kompyuta yako. Vigae hivi vitakuwa pia na taarifa mbalimbali kuhusu yaliyomo kwenye programu hiyo kwa mfano, barua pepe ngapi mpya zipo kwenye programu yako ya kupata barua pepe. Utaweza kusukuma skrini (kwa kutumia mausi kwa kompyuta au kidole kwa kifaa-kompyuta cha kiganjani) ili kupata huduma mbalimbali kama kugawa habari kwenye mitandao ya kijamii.
Kiolesura cha Metro |
Mtazamo Wa Soko la Windows 8 |
No Comment! Be the first one.