Unakumbuka lile sakata la mwaka 2017 la simu ya Samsung Galaxy Note 7 kukumbwa na tatizo kwa baadhi ya betri za simu hiyo kusababisha mlipuko kwa simu hizo? Kama ndio basi simu hizo ambazo baadae zilikusanywa na kutolewa toleo jipya lililoitwa Samsung Galaxy Note FE sasa kuna habari njema kwa watumiaje wake.
Ni kwamba sasa simu hizo zitaweza kupata sasisho la toleo la Android 9.0 Pie. Toleo hili ndio jipya kwa simu zinazotumia mfumo wa Android. Likiwa na maboresho mengi mazuri na ya kuvutia. Samsung Galaxy Note FE iliyozinduliwa Korea Kusini iliuzwa kwa baadhi ya nchi duniani hususani kwa wale ambao hawakuweza kusubiri toleo lingine la Samsung Note 9 au Galaxy S9/S9+.
Wakati Samsung Galaxy Note 7 inatoka ilikuwa na toleo la Android 6.0 Marshmallow na baada ya kuondolewa sokoni kisha kuletwa Galaxy FE (Fan Edition) ilikuja na Android 7.1 Nougat kisha kupokea masasisho ya Android 8.0 Oreo na kuhaidi kuruhusu masasisho ya Android 9 kuja mwezi Machi 2019 na sasa hilo limetimia.
Samsung Galaxy FE: Sasisho la uwezo wa kupakua Android 9 kwenye Samsung Galaxy Note 7. Sasisho hilo lina ukubwa wa GB 1.5.
Samsung Galaxy FE inafanana karibu vipengele vyote ambavyo Note 7 ilikuwanavyo isipokuwa nguvu ya betri ambapo toleo lililopita lilikuwa na 3500mAh wakati hili la sasa betri yake ina mAh 3200.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.