fbpx

Google Hangouts kufikia tamati ya kutumika

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Huduma mbalimbali za Google zimeripotiwa kufikia tamati baada ya muda fulani na safari hii Google Hangouts ipo kwenye mlolongo wa kutotumika tena.

Takribani programu tumishi mbili zinazomilikiwa na Google zimebainishwa kuacha kutumia kila moja katika kipindi/mwaka tofauti na hapa nazungumzia Google Plus ambayo itafungwa mwaka 2019 huku Google Hangouts ikifikia tamati mwaka 2020.

Google Hangouts ilianza kutumika mwaka 2013 ambayo kimsingi inatoa huduma ya mawasiliano (kwa maandishi/picha jongefu) kwenye Gmail lakini pia hata jumbe za kawaida kwa maana ya kwamba unaweza kutuma/kupokea ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwa mtu anayetumia mtandao wa simu.

tamati

Google Hangouts imeonekana kuwa mbadala wa watumiaji wa simu janja kwenye mfumo wa kutuma/kupokea jumbe kutokana na kuwa na vitu vingi vya kuvutia.

Google Hangouts inafikia ukingoni lakini bado tukiwa na programu kama Google Allo na Duo ambazo kimsingi zinavutia na kuwa na vikorombwezo kadha wa kadha.

Vyanzo: GSMArena, 9to5Google, The Verge,

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Simu ya Pixel 3A na 3A XL - Google waja na Simu ya Pixels kwa bei 'rafiki'
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.