Kampuni ya Bharti Airtel ya nchini India inayomiliki mtandao wa simu wa Airtel barani Afrika ipo njiani kuuza baadhi ya biashara zake za Afrika.
Kwa muda mrefu imesemekana kampuni ya Bharti haijapata faida katika nchi nyingi za Afrika ambazo mtandao wake wa Airtel unafanya kazi, na ikasemekana watauza huduma zao zote za barani Afrika muda si mrefu.
Masaa kadhaa yaliyopita kampuni hiyo imefanya mazungumzo na kampuni maarufu ya huduma za simu ya barani ulaya – Orange. Kampuni ya Orange inamiliki biashara za huduma ya simu katika nchi mbalimbali barani Ulaya na Afrika.
Kampuni ya Orange inamilikiwa kwa asilimia 32 na serikali ya Ufaransa huku asilimia airtnyingine ya umiliki ukiwa katika soko la hisa.
Je Tanzania ni moja ya nchi ambayo mtandao huo utauzwa?
Katika baadhi ya nchi ambazo wanafikiria kuuza biashara zake ni pamoja na Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville na Sierra Leone. Katika masoko ambayo mtandao wa Airtel unafanya vizuri inasemekana Tanzania ni moja wapo na hii inaweza ikawa ni moja ya sababu kuu ya kutouza.
Kigezo kikubwa katika maamuzi yao ni kujitaidi kuondoka katika mataifa ambayo wamekuta biashara ni ngumu na hawatengenezi faida.
Mtandao wa Airtel kupitia kampuni mama ya Bhartel Airtel uliingia Afrika rasmi mwaka 2010 baada ya kununua mtandao wa Zain afrika nzima kwa kiasi cha takribani Tsh Trilioni 20. Airtel inatoa huduma katika nchi 17 barani Afrika, lakini bado tokea ununuaji huo kufanyika bado hawajaweza kupata faida ya ununuaji huo.
Endelea kutembelea mtandao wako wa TeknoKona kwa habari mbalimbali kuhusu mitandao ya simu na teknolojia.
No Comment! Be the first one.