Tokea mwaka 2010 watu walianza piga picha pamoja na kuhariri (edit) picha hizo zikiwa katika mfumo wa mraba. App hii inajulikana kwa kiasi kikubwa kama instagram. Licha ya kampuni kufanya vizuri sana katika App ya simu.
Lakini bado wapo nyuma katika World wide web (www). Mabadiliko huko bado hayajawa makubwa kwani mpaka sasa unaweza ukaangalia ukurasa wako (profile) na kufanya marekebisho (settings) flani tuu
Pengine labda siku ya mtumiaji kuweza kuhariri picha yake na kutuma katika akaunti yake ndani ya www haitatokea. Lakini bado kampuni imechukua hatua kubwa kwa kuongeza kipengele cha ‘Tafuta’ (serach). kipengele hiki kinatumika tafuta watumiaji wengine na #Tag zote zilizoko instagram. Mfano unaweza ingia katika instagram.com na kisha pale kwa juu utaona kiboksi cha ‘Search’. Ukienda pale na kuandika TeknoKona, basi bila shaka itatokea akaunti ya teknokona.
Hii ni hatua nzuri sana ambayo imechukuliwa na istagram. Lakini pengine cha kushangaza ni kwa nini imechukua mda mrefu? Najua sio peke yangu nnaejiuliza hivyo. Huduma zingine kutoka mitandao kama vile FindGram na Websta amabazo zinawezesha watumaiji wa instagram kwa Desktop kutafuta (Search) watu na #Tags hazitahitajika tena kwani umuhimu wake utapotea.Kwanini mtu asumbuke kama anweza fanya kilakitu akiwa www.instagram.com
No Comment! Be the first one.